Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Njombe

Benki ya Maendeleo ya TIB imeunga mkono juhudi za uzalishaji wa nishati nchini kwa kutoa mkopo wa kiasi cha Dola za Kimarekani 400,000 kwa kampuni ya Nishati Lutheran (DKK) Investment Ltd inayotekeleza ujenzi wa Mradi wa Umeme wa Ijalanga ‘Small Hydro Eclectic Power Project (ISHEP)’ uliopo pembezoni mwa Mto Ijawala mkoani Njombe. 

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya TIB, Mkurugenzi Mtendaji, Joseph Chilambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa mradi huo imefanyika katika makao makuu ya Kampuni ya Lutheran Energy Company (DKK) Investment Ltd, iliyopo kata ya Tandala, kijiji cha Msisiwe Makete. wilayani Njombe. 

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB, Bw. Joseph Chilambo akizungumza wakati wa sherehe za uwekaji jiwe la msingi kwenye mradi wa umeme Ijangala ‘Min Hydropower Project’ zilizofanyika katika kijiji cha Msisiwe Wilayani Makete Mkoani Njombe. Mradi huo umefadhiliwa na mkopo kutoka Benki ya Maendeleo TIB, ruzuku kutoka kwa Wakala wa Nishati Vijini (REA) pamoja na wahisani mbalimbali wa Kanisa hilo. 

Chilambo alisema benki imetoa mkopo kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa mradi huo ambao utakuwa na uwezo wa kuzalisha kilowati 360. 

Alisema benki imechagua kufadhili mradi huo kwa kuwa unatarajiwa kuwa na matokeo chanya ya kiuchumi na kijamii ambazo zitachangia mpango wa nchi wa kusambaza umeme vijijini na kupunguza umaskini vijijini kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya uzalishaji umeme ili kuongeza tija katika shughuli za maendeleo nchini. 

Kulingana na pendekezo la mradi huo, mradi huo utaboresha hali ya maisha kwa kuboresha upatikanaji wa umeme kwa maendeleo ya biashara ndogo ndogo na matumizi ya nyumbani. 

Mradi wa Umeme wa Ijalala Small Hydro Eclectic Power sasa uko chini ya utaratibu wa Mpango wa Upanuzi wa Nishati Jadidifu Tanzania (TREEP) chini ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA). REA kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imeanzisha programu ya kusaidia maendeleo ya Miradi ya Nishati Jadidifu nchini Tanzania. 

TREEP imeundwa kama Programu ya Matokeo (PforR), inayounga mkono Mpango wa Kitaifa wa Umeme Vijijini wa serikali (NREP) kwa kuunganisha kwa ubunifu utoaji wa fedha moja kwa moja na utoaji wa matokeo yaliyoainishwa na kufikia malengo yake, ambayo ni pamoja na Kupanua upatikanaji wa umeme vijijini. 

Jiwe la msingi liliwekwa na Askofu wa Jimbo la Mashariki na Pwani, Dk Alex G. Malasusa akimwakilisha Baba Askofu, Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dk Fredrick Onael Shoo. 

By Jamhuri