Na Mwandishi wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Katika kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ajenda ya kuinua wanawake kiuchumi, Benki ya Mwalimu Commercial imezindua bidhaa mpya ya ‘Tunu’ kwa ajili ya Wanawake na Vijana .

Hayo yamebainishwa jijini Dar es salaam na Mkuu wa Kitengo cha ukuzaji biashara na masoko kutoka Benki hiyo,Leticia Ndongole katika halfa ya kusherekekea siku ya Wanawake duniani iliyowakutanisha Jukwaa la viongozi wanawake wa Mashirika ya umma, taasisi na wanasiasa wakongwe.

“Kwa mwaka 2024 tumeona tuweze kushirikiana na Taasisi za umma sambamba na kumuunga mkono Rais Dkt Samia katika ajenda ya kuinua wanawake”amesema Leticia.

Amesema wamekuwa wakitoa huduma kwa walimu Tanzania nzima pamoja na wanawake waliopo katika ngazi zote katika jamii.

Aidha ameongeza kuwa katika kuazimisha siku ya wanawake Dunia Machi 8 wameona ni vema kushirikina na wanawake p katika kuzindua bidhaa hiyo .

Vilevile amesema wanawake wamekuwa wakisukumwa na ajenda moja ya kumuwezesha ili kuharakisha maendeleo ya kiuchumi Kwa Taifa .

“Tumeona ni vema kuzindua bidhaa hii ya tunu tunaamini Kwa ushiriki wa wakuu wa Taasisi za umma tutaweza kuwafikia wanawake wengi katika ngazi zote “amesema na kuongeza:

“Asilimia kubwa ya wanawake ndio wamekuwa wakikuza uchumi hasa katika sekta binafsi…Kama Mwalimu commercial Bank tumeona tunaowajibu wa kuhakikisha kwamba tunaweza kuwasaidia wakinamama katika nyanja mbalimbali ikiwemo kuwaingiaza katika sekta ya fedha Kwa kuwapatia elimu katika upande wa kuwekeza na hatimaye kukuza biashara yao” amesema Leticia.

By Jamhuri