Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA)

Taarifa iliyotolewa leo novemba 13, 2023 na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu imeeleza kuwa;

Rais Samia amemteua Dkt. Jones A. Killimbe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Aidha amemteua Juma Hassan Reli kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Itakumbukwa kuwa Novemba 07 mwaka huu Rais Samia alivunja Bodi hiyo iliyokuwa ikiongozwa na Mhandisi Othman Sharif Khatib ambae alikua Mwenyekiti, pamoja na Makamu Mwenyekiti wake Khalfan Saleh Makamu

Wajumbe wa Bodi hiyo walikuwa ni;Dk Mzee Suleiman Mndewa, Fatuma Simba, Ikuja Abdallah, Batenga Katunzi na Rehema Jessica Khalid