JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Category: Siasa

Dk. Slaa ‘ammaliza’ Sitta

Tea/sept2

lead

 

*Amwanika alivyohaha kujiunga Chadema

*Aeleza alivyotumia Uspika kuasi CCM

*Afichua hotuba aliyoandaa kujitoa

 

Siri za mkakati wa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), zimeanza kuvuja.

OXFAM yaivuruga Loliondo

*Yazifadhili asasi kuvuruga amani Loliondo

*Yazichotea mamilioni kufanikisha vurugu


Shirika la Misaada la Kimataifa la Oxfam limejiingiza kwenye ufadhili wa vikundi na asasi za kiraia, zinazozua na kuchochea mgogoro kati ya Serikali na wafugaji wa jamii ya Kimaasai katika Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

Msekwa ang’olewa Bodi Ngorongoro

*Orodha ya kwenda Ikulu jina lake lakatwa

*Ukomo wake ni Oktoba 5 mwaka huu

*Kilio cha kina Telele, Sendeka chasikika

Jina la Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Pius Msekwa, halimo katika orodha ya majina ya watu wanaopendekezwa kushika wadhifa huo, JAMHURI imethibitishiwa.

URAIS 2015

 

*Vikumbo vyaanza uchaguzi NEC-CCM

*Matayarisho ya mitandao yapamba moto

*Sura mpya, waliopotea waanza kuibuka

*Kipimo cha kukubalika ni kwenye NEC

Harakati za kuwania nafasi mbalimbali, hasa ujumbe wa Halmashauri Kuu (NEC) ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), zimetafsiriwa kwamba ni maandalizi ya kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015.

Mkurugenzi: Ilala jitokezeni sensa

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilala, Gabriel Fuime, amewataka wakazi wa Ilala kujitokeza kwa wingi kushiriki sensa ya watu na makazi inayofanyika kuanzia Jumapili wiki hii. Fuime aliiambia JAMHURI mwishoni mwa wiki kuwa kuna umuhimu mkubwa wa wakazi wa Ilala kujitokeza kwenye sense, kwani bila kufanya hivyo mgawo wa fedha kutoka serikalini utapungua.

Ripoti ya majangili yatoka

*Wamo Polisi, Kada CCM, wafanyabiashara

*Vigogo Polisi Kigoma, Mugumu wahusishwa

 

Idara ya Ulinzi, Kitengo cha Intelejensia cha Mamlaka ya Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), imetoa ripoti ya ujangili iliyo na majina ya wahusika wakuu na namna wanavyolindwa na vyombo vya dola  nchini. JAMHURI imepata ripoti hiyo ya kurasa 30 iliyosainiwa na Mhifadhi wa Intelejensia, Renatus Kusamba.