Category: Maoni ya Mhariri
Hongera Wakenya, Tanzania tujiandae
Wiki iliyopita tumeshuhudia Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya, ikitangaza matokeo ya uchaguzi mkuu. Matokeo hayo yamempa ushindi Uhuru Kenyatta wa Muungano wa Jubilee. Mshindani wake wa karibu, Raila Odinga amekataa kutambua matokeo haya.
Wakenya heshimuni matokeo ya uchaguzi
Uchaguzi Mkuu wa Kenya ulimalizika jana kwa utulivu na amani, licha ya kuwapo kwa dosari ndogondogo, ikilinganishwa na wa mwaka 2007. Watu wengi duniani wameshuhudia na kusikia jinsi wananchi walivyojitokeza kwa wingi, kutumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia kuchagua viongozi watakaowaongoza kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Serikali imdhibiti mwekezaji huyu
Moja ya habari zilizobeba uzito wa juu katika gazeti hili ni ile inayomhusu raia wa Uswisi, Dk. George Hess, anayetuhumiwa kumiliki na kuuza ufukwe wa Amboni uliopo Wilaya ya Muheza, mkoani Tanga kinyume cha sheria.
Tutaijutia amani tunayoichezea
Kwa muda wa mwezi sasa nchi yetu ipo katika migogoro isiyomithilika. Yamekuwapo matukio yanayotia shaka iwapo sisi wazazi tuna hakika na tunachostahili kuwapatia watoto wetu. Kule Mwanza na Geita yametokea mauaji yaliyotokana na mapigano kati ya Wakristo na Waislamu wakigombea kuchinja wanyama.
Tuondokane na bima za magari
Kwa wiki nzima sasa kuna mjadala unaoendelea hapa nchini juu ya mpango wa kurekebisha viwango vya malipo ya bima ifikapo Machi mosi. Mpango huu unalenga hasa bima kubwa (premiums). Wanalenga kuweka viwango vya kati ya asilimia 3.5 hadi 9 kwa kila gari. Hawakuzungumzia suala la bima ndogo (third part).
Upungufu wa dawa, wafadhili ni hatari
Shirika lisilo la kiserikali linalofanya kazi ya kuboresha utawala bora, uwazi na uwajibikaji katika sekta ya afya na Ukimwi, SIKIKA, wiki iliyopita limetoa taarifa yenye kushtua juu ya upatikanaji wa dawa na wagharimiaji.