Wabongo roho mbaya hadi Ulaya?
Kuna watu huwa wanafikiria wenzao walio ughaibuni – Ulaya, Marekani au hata Mashariki ya Kati – ni wachawi. Halafu kuna wengine walikuwa wakisema kuwa labda waliotoka Tanzania na sehemu nyingine za Afrika kwenda huko na kupata maendeleo, walibebwa au ni kubarikiwa tu.