Na Mwandishi Wetu JAMHURI MEDIA Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amewataka watendaji na viongozi katika ngazi za mitaa wilaya na manispaa kutumia matokeo ya takwimu za Sensa katika kufanya maamuzi.

Chalamila ametoa agizo hilo leo Juni 28, 2023 jijini Dar es salaam wakati  wa uwasilishaji wa matokeo ya sensa kwa watu na makazi ya mwaka 2022 kwa watendaji wa kata, mitaa na wenyeviti wa Manispaa.

Chalamila amesema lengo la sensa duniani kote huwa  ni kupata taarifa za kidemografia, ambapo taarifa zake  huchakatwa ili ikuweza kufanya maamuzi ya kupanga maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

“Taarifa hizi zinachakatwa kuweza kuzalisha takwimu ambazo matumizi yake makuu ni kusaidia kufanya maamzi yanayohusu maendeleo ya watu kiuchumi kijamii n ahata kisiasa.”amesema Chalamila

Mkuu wa Mkoa huyo amesema,  zoezi la kuchakata na kutafsiri taarifa za sensa ni muhimu kwa nchi katika maandalizi ya mipango ya maendeleo na bajeti huanzia ngazi za chini kwenda juu.

Awali akizungumza kwa niaba ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Fausta Mtigiti amesema  uwasilishaji wa matokeo ya sensa kwa mkoa wa Dar ses Salaam umefanyika kwa awamu ya pili sasa,katika awamu ya kwanza ulifanika Machi 14, 2023 ambapo matokeo yake yalipitishwa bila uchambuzi wa kina.

“kama mtakumbuka kwamba maswali yetu ya sensa yalikuwa ni mengi lakini  matokeo yake tunayatoa kwa awamu, ndo tumeanza na idadi ya watu lakini pia tunaendelea tunaendelea na uchambuzi na mwisho wa siku matokeo yanapokamilika basi tunayaleta kwenu”amesema Fausta Mtigiti.

Aidha Chalamila amewasisitiza viongozi katika ngazi za halimashauri na wilaya kuzingatia mafunzo watakayopata katika semina hiyo ili kufahamu kwa undani matumizi sahihi ya takwimu Pamoja na kuelewa taarifa sahihi za watu ili kuwawezesha kupanga na kutekeleza  miradi ya kimaendeleo.

By Jamhuri