Na Severin Blasio, JamhuriMedia, Morogoro

Wananchi wameshauriwa kuacha tabia ya kununua dawa na kutumia bila ushauri wa daktari na badala yake waende kwenye kituo cha kutoa huduma wapate ushauri wa kitaalam.

Kauli hiyo imetolewa na mganga mfawidhi wa wa kituo cha huduma ya mama,baba na mtoto cha Susannah Wesley (Polyclinic) Dkt Bahati Faustine kwenye uzinduzi wa jengo la huduma ya mama,baba na mtoto.

Kituo hicho kinamilikiwa na kanisa la The United Methodiist Tanzania kilichopo kata ya Kihonda Maghorofani kilikuwa kinatoa huduma ya wagonjwa wanje (OPD) na kimeongeza jengo la mama,baba na mtoto (RCH)

“Kumekuwa na tabia iliyojengeka miongoni mwetu ya mtu anapojisikia kuumwa kwenda kwe nye duka la la dawa au tiba mbadalana kununua dawa kisha kuzitumia bila kujua anatibu nini.

“Na wengine huenda mbali zaidi na kuwapigia simu baadhi ya watoa huduma wa za afya na kuuliza aina ya dawa ya kumeza ili wapone jambo ambalo ni kinyume na kanuni za matibabu “amesema Dkt Faustine.

Dkt Faustine amesema utaratibu wa matibabu unawataka wananchi wanapojisikia wanaumwa kwenda moja kwa moja kwenye kituo cha huduma ili waonane na daktari ambaye atamsikiliza ,kumchunguza ,kumpima na baada ya kugundua ugonjwa atamwandikia dawa za kutumia.

Aidha Dkt Faustine ametoa shime kwa wazazi kujenga mazoea ya kuonana na wataalamu wa masuala ya uzazi kabla ya hawajapata ujauzito sambamba na kuhimiza umuhimu wa mama na mtoto kutumiza chanjo zote.

Ametoa changamoto ya kituo hicho kuwa ni kutopata kibali cha huduma ya mfuko wa bima ya afya,miundombinu ya barabara na ukosekanaji wa usafiri wa wagonjwa wanaohitaji rufaa.

Akijibu changamoto za kituo hicho,Mratibu wa huduma za afya Manispaa ya Morogoro Dkt Felister Stanslaus kwa niaba ya mganga mkuu amemuhakikishia daktari wa kituo cha Susannah wesley polyclinic kuwa serikali haitawaaacha nyuma wapo tayari kushirikiana nao katika kuongeza ufanisi katika kutoa huduma hiyo.

Naye mgeni rasmi Katibu tawala mkuu wa wilaya ya Morogoro Hilary Sagara ameppongeza Kanisa la The Unaited Methedist kwa kuweza kusaidiana na serikali katika kupanua huduma za afya

By Jamhuri