Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia,Chalinze

Halmashauri ya Chalinze , mkoani Pwani imepokea gari la Zimamoto na Uokoaji litakalosaidia wakati yanapotokea majanga ,kutoka kwa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ( SSF) Jenifa Shirima.

Akiongea kwa niaba ya wananchi wa Chalinze , Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alimshukuru Mrakibu Mwandamizi kwa niaba ya Serikali kwa kuona kuwa katika mipango ya Serikali Chalinze iwe moja ya maeneo ya kipaumbele katika uhitaji huo.

Ridhiwani alikumbusha kilio cha muda mrefu cha wananchi wa Chalinze na majanga yaliyo wahi kuwakuta na ujio wa gari hili ni ukombozi mkubwa kwao.

Awali, Mrakibu Mwandamizi Jenifa alimpongeza mbunge kwa kuwasemea wananchi wake na gari hilo ni utekelezaji wa maombi yake.

Alimuahidi mbunge kuendelea kutatua kero za Zimamoto katika Halmashauri zote mkoa na kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Chalinze, Possi kwa kuwapatia Kiwanja ambacho watajenga Jengo la zimamoto la wilaya na ofisi zao.

Kadhalika alimhakikishia mbunge kuwa Serikali inajipanga kwa ajili ya ujio wa gari kubwa la wilaya hiyo.

Wananchi wa Chalinze, waliishukuru Serikali kwa kutatua kero hii ya muda mrefu na kuahidi kulitunza

By Jamhuri