Chongolo aendelea na ziara Bahi mkoani Dodoma

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo amewasili wilayani Bahi, Dodoma ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kuimarisha uhai wa Chama pamoja na kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2020-2025.
Katika ziara hii wilayani Bahi ameongozana na Mjumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi Gavu.