Na Mwandishi Wetu, JanhuriMedia

MPANGO wa Taifa wa Damu Salama kupitia Kanda ya Mashariki inayojumuisha Mikoa ya Dar Es Salaam, Pwani na Morogoro imekabidhi kadi za Kielektroniki kwa wachangiaji vinara zaidi ya 96.

Tukio hilo la kipekee lililofanyika mapema Septemba 25,2023 Mchikichini Ilala, Dar Es Salaam .

Awali akikaribisha wadau na mashujaa vinara wachangia damu katika tukio hilo waliowakilisha wengine wa Kanda ya Mashariki kupokea kadi hizo, Meneja wa Kanda hiyo, Dkt. Pendaeli Sifueli amewapongeza wachangia damu kwa kuendelea kujitokeza kwani uchangiaji wao huo uokoa maisha kwa Wanchi wengi wa Tanzania.

“Shukrani kwa Taasisi zote kufika hapa kuungana nasi pamoja na wachangia damu katika tukio hili.

Ikumbukwe wahitaji wakubwa ni wamama wajawazito, watoto chini ya miaka 5, lakini pia magonjwa kama sicle seli, na magonjwa mengine sugu ni wahitaji wakubwa wa damu.” amesema Dkt. Pendaeli.

Aidha, amemfahamisha mgeni rasmi juu ya changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo masuala ya usafiri kwa watenda kazi kwenda kwenye maeneo ya uchangiaji, lakini pia vifaa vya utendaji kazi lakini wanapambana kuhakikisha wanakusanya damu ilikuokoa maisha” Amesema Dkt. Pendaeli.

Aidha, amesema kuwa kadi hizo wametoa kwa awamu kutokana na kufikia vigezo hivyo vya kupatiwa kadi za mchangia damu Kielektroniki ambazo zina thamani kubwa.

“Hizi kadi ukienda kokote itasoma na utaitumia katika kupata huduma.
Kadi hii pia inaenda kupunguza matumizi ya makaratasi, kwani itatumika kisasa zaidi katika mufumo maalum” amesema Dkt. Pendaeli.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika tukio hilo Mwenyekiti wa Khoja Shia Ithna-Asheri Jamaat Tanzania, Mohamed Raza Dewji ameshukuru kuwa mgeni kwa tukio hilo kwani anathamini kampeni ya uchangiaji damu.

“Tunathamini zoezi la uchangiaji damu.
Na ndo maana kupitia Hospitali ya Ibrahim Hajj ya Mjini kila mwezi tunaendesha zoezi la uchangiaji damu.

tutatembea, tutakimbia kwa pamoja katika kuungana na wadau kwenye uchangiaji wa damu… naamimi taasisi za uchangiaji damu naona hamasa ya kushirikiana nao kwa pamoja siku za baadae ilikumuokoa mwananchi muhitaji wa damu salama” Amesema Dewji.

Aidha, amesema wameanzisha mpango maalum wa wachangia damu kupata elimu ya mchangia damu na ameona inaleta mafanikio.

Katika tukio hilo taasisi mbalimbali zimeweza kushiriki zikiwemo JAI na zingine nyingi.

By Jamhuri