Na Helena Magabe Jamuhuri media Mwanza.

Waandishi wa habari wametakiwa kutumia takwimu wanapoandika habari ili kuongeza uelewa katika kazi zao kwa mujibu wa matokeo ya sensa ya mwaka 2022.

Wito huo umetolewa na mgeni rasmi MKuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi ambaye amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Amosi Makala kwenye ufunguzi wa mafunzo ya takwimu ya siku mbili yaliyofanyika jijini Mwanza.

Amesema waandishi wa habari wanatakiwa kusambaza matokeo ya sensa ya watu na makazi ili kuwafikia wananchi ili wajue manufaa ya sensa.

Kamishina wa sensa 2022 Anna Makinda amewapongeza waandishi wa habari kwa jitihada zao kuhamasisha wananchi kuhesabiwa.

Amesema matokeo ya sensa ya mwaka 2022 katika ofisi ya Taifa ya Takwimu yanahusisha vyombo vya habari ili kupata uelewa mpana wa kutumia wajibu wa kusambaza kwa kuchakata na kuelimisha Jamii kwa kutumia takwimu.

Meneja wa Takwimu mkoani Mwanza Goodluck Lyimo, amesema matokeo ya sensa ya mwaka ya watu na makazi 2022 yanaonyesha idadi imeongezeka kufikia watu milioni 61.7 sawa na ongezeko la asilimia 3.2 kwa mwaka kutoka milioni 44.9 kwa mwaka 2012.

Amesema Tanzania bara imeongeza idadi ya Watu kutoka milioni 43.6 mwaka 2012 hadi watu milioni 59.9 mwaka 2022 ambapo lwa Zanzibar idadi ya watu imeongezeka kutoka milioni 1.3 2012 na kufikia watu milioni 1.9 sawa na ongezeko la asilimia 3.7

Kwa wa upande wake mratibu wa mavunzo na mwenzeshaji Said Ameil amezungumzia majukumu ya ofisi ya Taifa ya takwimu (NBS) kuwa inatumia Sheria ya NBS ya sura 351 ambayo ilibadilishwa 26 machi 1999 yenye ina miundo miwili ambayo inashughulikia uchumi,mazingira na jamii.

By Jamhuri