Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Njombe

Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa ametoa wito kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya ukimwi kuacha kuogopa kutumia dawa za kufubaza maambukizi kwa kuwa Serikali imetatua changamoto ya kukosekana kwa dawa hizo huku akiwataka kuacha kuchanganya ARV’s na dawa za kienyeji.

Aidha mkuu huyo wa wilaya mara baada ya kukagua shughuli za maendeleo zinazofanywa na vikundi vya WAVIU kupitia konga za Halmashauri ya Wilaya ya Njombe,amesema ni hatari kwa watu kunywa dawa kwa kificho kwa kuwa wamekuwa wakijisababishia matatizo makubwa.

“Ukiacha dawa ghafla kuna madhara makubwa na wengine wanachanganya na dawa za kienyeji,lakini kuna hawa wanaokunywa dawa kwa kificho hii ni hatari zaidi kwasababu unapoenda kliniki unapimwa na wataalamu wanajua kama kuna haja ya kukubadirishia dawa,wengine wamefikia hatua ya kununua wenyewe dawa za nje zisizokuwa na kipimo na kupata madhara”amesema Kissa Kasongwa

Mganga mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Dkt.Suke Magembe ametoa ushauri kutumiwa dawa zilizothibitishwa na mkemia mkuu ili kuepukana na madhara

By Jamhuri