Hamisi mobeto akiwa na Diamond

Mwanamuziki Diamond Platnumz na mzazi mwenzake, Hamisa Mobetto wamefika katika Mahakama ya Hakimu Makazi Kisutu jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kusikiliza shauri linalohusu matunzo ya mwanao.

Novemba 10 ,2017 Hakimu Devotha Kisoka wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa Watoto alitupilia mbali kesi hiyo juu ya matunzo ya mtoto Prince Abdul.

Diamond aliwasilisha pingamizi dhidi ya kesi hiyo iliyofunguliwa na Mobeto akidai kuwa kesi hiyo imefunguliwa kwa kutumia kifungu ambacho si sahihi. Hoja ambayo ilipingwa na Mobeto.

Mobeto alifungua kesi hiyo mahakamani hapo, pamoja na mambo mengine anaiomba matunzo ya mtoto waliozaa na msanii Diamond.

2993 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!