Mkutano wa Kumi na Moja wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unafanyika leo, Mei 23, 2024 katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mgeni rasmi ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.

Mkutano huo ulioanza Mei 20, 2024, utahitimishwa Mei 25, 2024 unalenga kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa kada hiyo ikiwa ni pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia maadili katika maeneo yao ya kazi.

Kaulimbiu ya mkutano huo ni “MAFANIKIO HUANZA NA UAMUZI BORA WA UTENDAJI, TUTUMIE MUDA VIZURI KWA KUFANYAKAZI NA KULETA TIJA”

Please follow and like us:
Pin Share