Na Helena Magabe, JamhuriMedia,Tarime

Halmashauri ya Mji Tariime Kwa kushirikiana na Benki ya Equity wametoka semina fupi kwa vikundi mbalimbali vya huduma ndogo vilivyopo Tarime Mjini.

Lengo la semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Sky ni kuwajengea uwezo Wana vikundi juu ya kujitunzia akiba pamoja na kubaini changamoto wanazokabiliana nazo na namna ya kuzitatua.

Afisa maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Mji Tariime Vitus Gwanko amesema Halmashauri ina vikundi 457 na bado wanaendelea kusajili ambapo kwa siku ya leo walipanga kukutana na vikundi 50 ila kutokana na sababu mbali mbali vimehudhulia vikundi 44.

Afisa Mahusiano biashara Equity Benki Boniphace Manota akionyesha kadi ya visa ya Equity Benki

Gwanko amesema amebaini kuwa wanasajili vikundi kwa katiba lakini katiba hazifuatwi ambapo amesema kila kikundi ni lazima kiwe na katiba na kila mwanachama awe na katiba itakayo mwogoza ili kuepusha migogoro mbali mbali inayojitokeza kwenye vikundi na kuongeza kuwa baada ya Pasaka wanaanza kuwasaka wasumbufu wa marejesho.

Amewataka wenyeviti wa vikundi kuacha kutengeneza makundi, sheria ziwe wazi faini zinazopigwa ziendane na zilizoko kwenye katiba na vile vile waache tabia ya kubadirisha mihutasali bali kila jambo linalofanywa kwenye kikundi lifanyiwe maamuzi na wanachama wote.

Amesema kiongozi yoyote ambaye hafuati utaratibu wa vikundi hawezi kulinda mali za vikundi atamwondoa hata kama anechaguliwa na wana kikundi na itafika wakati katika chaguzi zao Maafisa toka Halmashauri watashiriki kama wasimamizi wa uchaguzi ili kupata Viongozi sahihi.

“Unakuta kuna makundi machache yananufaika ukifanyika uchaguzi wanasema Mwenyekiti abaki huyo huyo wakati sisi tunataka kuwajengea uwezo watu wote ili mtu yeyote aweze kusimamia vizuri kikundi” amesema Gwanko.

Aidha amekemea tabia ya mtu mmoja kuwa na tamaa ya kuwa vikundi vitano au zaidi na badala yake awe na kimoja au viwili ambavyo anakuwa na uwezo wa kurejesha na kuongeza kuwa kikundi kikivunjika taarifa ya mhutasali itolewe Halmashauri ili kiodolewe kisionekane kwenye mfumo wakati kimekufa.

Mwezeshaji toka Equity Benki Said Chamwande ameelezea namna ambavyo Mwanachama anaweza kujiwekea akiba ya matumizi ya baadae kupitia Benki yao kwani akiba hiyo inaweza kumsaidia kwenye matatizo ya dharula.

Afisa maendeleo ya Jamii Vitus Gwanko.

Amesema wengi wanaogopa kutunza akiba Benki na kuona ni Bora watunze kwenye mchago,kwenye godoro au kwenye kibubu lakini Benki yao ni kibubu cha kisasa kwani benki ina akaunti zisizokuwa na makato na kuwa memba wa benki ya Equity inakupa fursa zaidi ya kufurahia huduma zitolewazo kama vile mikopo na bima, hivyo kukupa suluhisho halisi la mahitaji yako ya kifedha

Aidha amesema pia miongoni mwa faida za kuwa na akaunti ni kupata gawio la kila mwaka kulingana na mwingiliano wa fedha ambapo wana uwezo wakukopesha vikundi pamoja na mtu mmoja mmoja kulingana uhitaji wake na biashara aliyo nayo na kuongeza kuwa mchakato wa kupata mkopo ni ndani ya siku 7.

Afisa Mahusiano biashara wa Benki ya Equity Boniphace Manota amesema anatoa huduma mbali mbali za vikundi hapa Tarime ambapo wana mawakala wao wawili na ukiwa kadi ya visa ya Equity Bank una uwezo wa kutoa pesa kwenye Benki yoyote vile vile wanapatikana TPB Benki Tarime Mjini kwa huduma kila siku.

Mwalimu wa Vikundi (Mwezeshaji) Tarime Mjini Gemma John Marwa

Amesema kadi hiyo unaiwekea pesa harafu unaweza kuitumia kwenye matumizi yako mbali mbali kwa kutoa pesa yako kwenye ATM ya Benki yoyote Nchini hivyo inarahisisha huduma hasa pale mtu anapokuwa amepata dharula.

Aidha amesema kwenye akaunti ya jijenge mteja anaweza kujiwekea marengo ya kujiwekea akiba ndani ya miezi sita au mwaka bila kutoa na kujitegenezea faida kwa akiba aliyojiwekea.

Mmoja wa Walimu wa Vikundi Tarime Mjini (Mwezeshaji) Gemma John Marwa amesema kuwa kuna changamoto nyingi kwenye vikundi japo hazijasemwa hasa kwenye swala la mikopo na marejesho.

Amesema Wanachama wengi wamekuwa wakishindwa kurejesha mikopo kulingana na wingi wa Vikundi kwa sababu kina Mama wengi Wana vikundi vingi na wanashindwa kuviacha kulingana na uchumi wao kuwa mdogo lakini mikopo waliyo nayo ni mikubwa sana

Mwezeshaji toka Equity Benki Said Chamwande.

Aidha amesema hali hiyo inasababisha kuchelewesha marejesho yanayofuata kwa hiyo amewaomba Wana vikundi waangalie pesa wanavyokopa na wanavyo rejesha.

Askofu wa Kanisa la NAZARETHI Thobias Oluochi Agdeck mmoja wa Washiriki wa semina amesema tatizo Ofisi ya maendeleo ya Jamii inasajili kisheria lakini zinabadirishwa na sheria zinazokuwa zimetungwa sio zinazotumika kwenye vikundi.

Aidha ameuliza utaratibu unatakiwa kufanyika kwenye mikopo ya Equity Bank kuomba mkopo wa mitambo mfano ya kuchimba kisima, vifaa mbali mbali au aseti unafanyika kwa utaratibu gani.

Naye Alphonce Alkad (Babu wa Mjini) amewaka Benki ya Equity kuwa na tawi lao Tarime ili kuwarahisishia Wanachama kukopa ambapo amesema, licha ya kuwa na mawakala wawili haitoshi wapanue wigo kama walivyo Dar es salaam na Mwanza wafungue tawi na Tarime.

By Jamhuri