Na Jumanne Magazi

Makamo Mwenyeki wa Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa mitaji ya Umma (PAC), Deus Sangu amesema kamati yao imeridhika uwekezaji na utekelezaji wa mradi wa Reli ya mwendokasi SGR.

Ameyasema hayo leo Machi 27,2024 wakati walipofanya ziara ya ukaguzi mradi ujenzi wa Reli ya SGR, sambamba na kuangalia majaribio ya treni hiyo kabla ya kuanza safari rasmi, mwezi Julai mwaka huu.

Sangu amesema kupitia kamati yao “tumeridhika pasipo na shaka namna uwekezaji mkubwa na usimamizi wa Hali ya juu uliofanywa na Serikali kwa mradi huo ambao unaakisi thamani ya pesa za Watanzania”

Aidha Sangu ameseme kwanza kama kamati wameridhika na uwekezaji umetekelezwa kwa viwango bora na unaovutia kwa watanzania.

Sangu amesema “Mradi huo utakuwa na faida nyingi sana kwanza kwenye utekelezaji wake umezalisha ajira za Moja kwa zipatazo elf 30,000 huku zile zisizo rasmi zaidi ya 150,000, ambazo zimezalisha kipato cha bilioni 350.

Sangu ameendelea kusema mara mradi huo utakapoanza utaweza kupunguza zaidi nusu ya muda ambao unatumiwa na mabasi yanatumia kutoka Dar es salaam mpaka Morogoro au Dodoma.

Vilevile, makamo mwenyekiti huyo amesema gharama za usafirishaji wa mizigo utakwenda kupunguza kwa zaidi ya asilimia 40 kutoka hivi sasa.

Amesema kwa jinsi walivyoona kama kamati maelekezo ya Rais Dkt,Samia Suluhu Hassan ambaye ameliagiza Shilika la Reli Tanzania (TRC) kwamba ifikapo mwezi Julai mwaka huu, reli hiyo iwe imeanza kufanya kazi kwa muda uliopangwa.

Katika hatua nyingine Sangu ameipongeza Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa iliyofanyika pia kwa kutoa fedha nyingi ili kufaniikisha mradi huo.

Aidha Sangu amesema mradi huo wa ujenzi wa mtandao wa reli nchini umeighalimu Serikali kiasi cha Dola biloni 10 sawa na Shilingi Trioni 23 fedha za kitanzania ambapo,hadi sasa Serikali imeshatoa asilimia 40 ya fedha jambo linalopelekea mradi huo kuendelea kukamilika.

Bw Sangu ametoa rai yake kwa Watanzania kukutumia mradi huo kwa lengo la kujiongezea kipato kwa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla sambamba na kutunza miundombinu ya teli na treni kwa ujumla iliiweze kudumu kwa kizazi na vizazi vijavyo.

Vilevile Sangu ameipongeza TRC, kwa usimamizi mzuri kwa mkandarasi ilikuhakikisha mradi huo unakamilika lakini pia ametoa rai kuwa kwa shirika hilo kutunza miundombinu lakini pia kuwasimamia wakandarasi ili kukamilisha mradi huo.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Shirika la Reli Tanzania TRC, Ali Karavina ,amesema wao kama shirika wamekamilisha kila kitu iliyobaki ni sehemu ndogo ya vipande viwili vya kutoka Dar es Salaam morogoro na Dar es Salaam Dodoma kwa vipande vilivyobaki.

Vilevile, Karavina amezungumzia suala la bei ya nauli ambapo amesema swala Hilo tayari lipo kwenye Mamlaka husika ikiwemo Ratra, hivyo amewaasa watanzania kuwa na subira wakati swala Hilo linafanyiwa kazi.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa TRC, Masanja Kungu Kadogosa ameishukuru kamati ya uwekezaji ya (P.A.C), na kusema kamati hiyo ni muhimu sana kwao, hivyo kitendo Cha kamati hiyo kuridhika inaashiria kuongezeka kwa fedha nyingine za mradi huo katika bajeti ijayo.

By Jamhuri