Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imevifungia vituo 3 vya uuzaji mafuta kwa muda wa miezi sita Camel Oil- Gairo Petrol Station chenye leseni namba PRL 2019-164,PETCOM-Mbalizi Petrol Station chenye Lessen namba PRL 2023-025,Rashal Petroleum Ltd – Mkalama chenye Leseni namba PRL 2019-034 huku vitatu vikiendelea kuchunguzwa kwa ajili ya hatua zaidi.

Akizungumza leo Septemba 18, 2023 na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile, amesema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na changamoto ya uhaba wa mafuta iliyotoke Agosti na Septemba,2023 ambapo baadhi ya wafanyabiashara wenye vituo kuficha mafuta kwa maslahi yao kusubiria bei kupanda hivyo wananchi kupata usumbufu wa kufanya shughuli zao za kiuchumi.

Hata hivyo amebainisha kuwa kutokana na ufichaji wa mafuta EWURA imevichukulia hatua vituo 8 ambavyo vimejihusisha na tabia ya kuhodhi mafuta ambapo Septemba 4 ,2023 EWURA ilivifungia vituo viwili vya CAMEL OIL MSAMVU MOROGORO na MATEMBA CHA TURIANI leo hivyo vitatu na vitatu vitatu vipo katika uchunguzi kwa ajili ya hatua zaidi

“Kwa mujibu wa Sheria ya Petrol sura Na 392 Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA ), imepewa jukumu la kudhibiti masuala ya mafuta pamoja na mambo mengine kuhakikisha kuna upatikanaji wa mafuta wakati wote na imepewa mamlaka ya kuwajibisha Vituo vinavyokiuka taratibu za leseni zao”amesema Dkt James.

Mkurugenzi Mkuu amewasisitiza wafanyabiashara kutambua kuwa biashara ya mafuta siyo holela kwani leseni zinazotolewa wajibu wa kutekeleza na EWURA inafuatilia utekelezaji wa Leseni zilizotolewa ikiwemo kwa wenye maghala,wamiliki wa vituo,na wafanyabiashara wa mafuta inapotokea masharti ya leseni hayazingatiwi hatua lazima zichukuliwe.

“Hata kama tukimkuta mdau wa mafuta anafanya kinyume na taratibu za leseni yake kisheria anapewa notisi ya siku 21 ajitetee kwa maandishi na utetezi ukipokelewa wajibu wa EWURA ni kuchambua Utetezi pale endapo itajiridhisha pasipo shaka hatua stahiki zitachukuliwa ” amesema Dkt.Andilile.

Aidha onyo limetolewa kwa wafanyabiashara, wenye vituo Mlmaghala ya mafuta kutohodhi mafuta kwani kumekuwa na tabia kila bei zinapoelekea kupanda wanapata jaribu la kuficha mafuta kusubiri bei mpya hivyo bado vijana wanaendelea kuchunguza na atakayethibitika hatua kali za kisheria zitachukuliwa .

By Jamhuri