Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imevifungia vituo viwili vya Mafuta GAPCO Tanzania Limitedi Moshi Service Station,leseni no PRL-2023-104 na Anwar Saleh BakhamisT/A Serious Oil Petrol Station,Leseni na PRL-2019-228 kwa miezi 6 kosa la kuhodhi Mafuta kati ya Mwezi Julai na Agosti 2023
Taarifa hiyo imetolewa leo Oktoba 27 jijini Dar es Salaam na Afisa Mawasiliano na Uhusiano EWURA Titus Kaguo, ambapo amesema ufungiaji wa vituo hivyo ni mwendelezo wa uchunguzi vituo vingine zaidi ikiwa ni pamoja na kuwapa fursa kuwasilisha utetezi wao ndani ya siku 21 baada ya kupitia utetezi wao EWURA ilijiridhisha pasipo shaka na kutoa adhabu hiyo vituo hivyo .
“Kwa kuvifungia vituo hivi viwi leo hadi sasa itakuwa imefikia vituo 11 na bado uchunguzi unaendelea kwa hituo vingine kwani tumekuwa tukotoa maonyo mara kwa mara lakini makosa ni yale yale yanajirudia ukiwatoza faini wanatoa bila kujali hivyo sisi EWURA hatuna shida na fedha zao tunawafungia tujajua kufanya hivyo hawezi kurudia tena”amesema Kaguo.
Kaguo amesema kwa mujibu wa sheria ya Petrol sura na 392 EWURA ina jukumu la kuhakikisha upatikanaji wa mafuta wakati wote na katika maeneo yote hivyo Mwezi Julai 2023 pamoja na kuwepo kwa changamoto ya upungufu wa mafuta katika maeneo mbalimbali ilichangiwa na baadhi ya wamiliki wa vituo vya kuuzia mafuta kwa makusudi kabisa kuamua kuhodhi mafuta ili kujipatia maslahi haramu ya kibiashara ikiwemo faida kubwa kutokana na ongezeko la bei za mafuta kinyume na sheria kanuni na miongozo inayosimamia bishara nchini.
Aidha EWURA imetoa onyo kwa OMCs na wamiliki wa vituo vya Mafuta kwani serikali inafuatilia suala hilo kwa karibu kupitia vyombo vyake mbalimbali na kituo kitakachobainika kinavunja sheria na kanuni hatua kali zitachukuliwa dhidi yao ikiwamo kuwafutia leseni ya biashara zao au kuwafungia