Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za  bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano, tarehe 6 Septemba 2023 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Septemba 2023, bei za rejareja za mafuta  katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama ifuatavyo: 

Mkoa Petroli Dizeli Mafuta ya Taa
TZS/Lita
Dar es Salaam 3,213 3,259 2,943
Tanga 3,259 3,305 2,989
Mtwara 3,285 3,332 3,016

Mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Septemba 2023 yanatokana na kupanda kwa  gharama za mafuta katika soko la dunia kwa hadi 21%, gharama za uagizaji wa  mafuta hadi 62% ikilinganishwa na mwezi Agosti, 2023 na maamuzi ya kisiasa katika  nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+). Bei za mafuta katika miji, wilaya na  mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 1 na bei za mafuta kwa  wafanyabiashara wa jumla ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 2.  

Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei  zinazooneshwa katika Jedwali Na. 1. Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa  jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 2. Hatua kali  za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili. 

EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na  rejareja pamoja na jamii kuzingatia yafuatayo: – 

  1. a) bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia  simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.  Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa  nchini. 
  2. b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za  bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea  kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.  
  3. c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya  ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya  bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni  za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2023 zilizotangazwa kupitia

Gazeti la Serikali Na. 421 la tarehe 23 Juni 2023. 

  1. d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika  mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya  kibiashara vinavyotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua,  wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta  kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka  mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa  kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni  husika. 
  2. e) Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo  kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe  wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya  mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti  kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa  bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora  unaotakiwa. Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za  Serikali zitokanazo na mauzo ya bidhaa za mafuta ya petroli. 

JEDWALI 1: BEI KIKOMO ZA REJAREJA KWA SHILINGI/LITA

MjiBei Kikomo
Petroli Dizeli Mafuta ya Taa
Dar es Salaam 3,213 3,259 2,943
Arusha 3,297 3,343 3,027
Arumeru (Usa River) 3,297 3,343 3,027
Karatu 3,315 3,362 3,046
Longido 3,308 3,354 3,038
Monduli 3,302 3,349 3,033
Monduli-Makuyuni 3,307 3,354 3,038
Ngorongoro (Loliondo) 3,388 3,435 3,119
Coast (Kibaha) 3,217 3,264 2,948
Bagamoyo 3,224 3,270 2,954
Bagamoyo (Miono) 3,254 3,301 2,985
Bagamoyo (Mbwewe) 3,235 3,282 2,966
Chalinze Junction 3,227 3,273 2,957
Chalinze Township (Msata) 3,231 3,277 2,962
Kibiti 3,233 3,280 2,964
Kisarawe 3,220 3,266 2,950
Mkuranga 3,222 3,269 2,953
Rufiji 3,240 3,287 2,971
Dodoma 3,271 3,318 3,002
Bahi 3,279 3,325 3,009

 

MjiBei Kikomo
Petroli Dizeli Mafuta ya Taa
Chamwino 3,267 3,313 2,997
Chemba 3,298 3,344 3,029
Kondoa 3,304 3,351 3,035
Kongwa 3,269 3,315 2,999
Mpwapwa 3,273 3,319 3,003
Mpwapwa (Chipogoro) 3,285 3,331 3,015
Mtera (Makatopora) 3,290 3,337 3,021
Mvumi 3,278 3,324 3,009
Geita 3,378 3,425 3,109
Bukombe 3,367 3,414 3,098
Chato 3,399 3,446 3,130
Mbogwe 3,416 3,463 3,147
Nyang’hwale 3,393 3,440 3,124
Iringa 3,277 3,323 3,007
Ismani 3,282 3,328 3,013
Kilolo 3,281 3,328 3,012
Mufindi (Mafinga) 3,287 3,333 3,017
Mufindi (Igowole) 3,295 3,342 3,026
Kagera (Bukoba) 3,428 3,475 3,159
Biharamulo 3,402 3,449 3,133
Karagwe (Kayanga) 3,445 3,491 3,175
Kyerwa (Ruberwa) 3,450 3,497 3,181
Muleba 3,428 3,475 3,159
Ngara 3,416 3,462 3,147
Misenyi 3,437 3,483 3,167
Katavi (Mpanda) 3,370 3,417 3,101
Mlele (Inyonga) 3,352 3,399 3,083
Mpimbwe (Majimoto) 3,390 3,436 3,120
Tanganyika (Ikola) 3,388 3,435 3,119
Kigoma 3,375 3,422 3,106
Uvinza (Lugufu) 3,365 3,412 3,096
Muyobozi Village (Uvinza) 3,374 3,420 3,104
Ilagala Village (Uvinza) 3,376 3,422 3,106
Buhigwe 3,374 3,420 3,104
Kakonko 3,376 3,422 3,106
Kasulu 3,384 3,431 3,115

3

MjiBei Kikomo
Petroli Dizeli Mafuta ya Taa
Kibondo 3,382 3,428 3,112
Kilimanjaro (Moshi) 3,286 3,333 3,017
Hai (Bomang’ombe) 3,290 3,336 3,020
Mwanga 3,279 3,326 3,010
Rombo (Mkuu) 3,307 3,354 3,038
Same 3,273 3,319 3,003
Siha (Sanya Juu) 3,293 3,339 3,024
Lindi 3,272 3,318 3,002
Lindi-Mtama 3,290 3,336 3,020
Kilwa Masoko 3,246 3,293 2,977
Liwale 3,292 3,339 3,023
Nachingwea 3,301 3,347 3,031
Ruangwa 3,302 3,349 3,033
Manyara (Babati) 3,335 3,382 3,066
Hanang (Katesh) 3,346 3,392 3,076
Kiteto (Kibaya) 3,346 3,393 3,077
Mbulu 3,348 3,394 3,078
Simanjiro (Orkasumet) 3,367 3,414 3,098
Mara (Musoma) 3,378 3,425 3,109
Musoma Vijijini (Busekela) 3,391 3,438 3,122
Rorya (Ingirijuu) 3,385 3,432 3,116
Rorya (Shirati) 3,393 3,440 3,124
Bunda 3,370 3,416 3,100
Bunda (Kisorya) 3,382 3,429 3,113
Butiama 3,376 3,422 3,106
Serengeti (Mugumu) 3,387 3,433 3,117
Tarime 3,387 3,434 3,118
Tarime (Kewanja/Nyamongo) 3,393 3,439 3,123
Mbeya 3,320 3,366 3,050
Chunya 3,329 3,376 3,060
Chunya (Makongolosi) 3,335 3,381 3,065
Chunya (Lupa Tingatinga) 3,336 3,383 3,067
Kyela 3,336 3,382 3,066
Mbarali (Rujewa) 3,304 3,350 3,034
Rujewa (Madibira) 3,317 3,364 3,048
Rujewa (Kapunga) 3,314 3,360 3,044

By Jamhuri