Mchezaji wa Yanga Feisal Salum Abdallah ‘Fei toto’ amewasili katika ofisi za shirikisho la mpira wa miguu Tanzania ‘TFF’ karume, jijini Dar es salaam mapema ya leo kuwasilisha maombi ya kulitaka shirikisho hilo kuuvunja mkataba wake na waajiri wake Yanga Sc.

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu shauri lake litupiliwe mbali, Feisal amewasili katika ofisi za TFF akiwa na barua ya kuomba mkataba wake na klabu ya Yanga uvunjwe akiongozana na mwakilishi wa Jasmin Razack.

Jasmin amesema ana imani kubwa sana na TFF kwasababu Ndio chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba wa mchezaji, ana imani TFF watalipokea ombi la Feisal na kulishughulikia.

“Nina imani kubwa na TFF, Feisal ameleta ombi lake kwa mara ya kwanza nina imani litashughulikiwa kwasababu TFF Ndio chombo pekee kinachoweza kuvunja mkataba wa mchezaji”. Alisema Jasmin.

Ni takribani miezi miwili sasa tangu Feisal aone Kane uwanjani akiwa na timu ya Yanga kwasababu ya mgogoro uliopo kati ya Feisal na klabu ya Yanga Sc huku chanzo kikielezwa kuwa ni ukiukwaji wa masharti ya kimkataba.

Hata hivyo Jasmin ameonekana kusaidia wachezaji wengi wanapokuwa kwenye migogoro na timu zao akiwemo Emmanuel Ebboue, Simon Msuva, na Wilfred Bony.

By Jamhuri