Klabu ya Singida Big Stars kwasasa inajulikana kama Singida Fountain Gate baada ya matajiri wa Fountain Gate kuinunua klabu hiyo.  

Singida Big Stars inashiriki ligi kuu Tanzania bara ‘NBC’ ikimaliza msimu katika nafasi ya nne na kukata tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho kimataifa msimu ujao.

Akizungumza na waandishi wa habari Rais wa Singida Fountain Gate Japhet Makau amesema wamechukua asilimia 100 ya umiliki wa Singida Big Stars.

Makau amesema wamefuata katiba na taratibu zote za usajili

ambapo kwasasa klabu hiyo inamilikiwa na mtu binafsi na sio timu ya wanachama.

Hata hivyo Makau amesema pamoja na kumiliki klabu hiyo kwa asilimia 100 bado klabu ya Fountain Gate itakuwepo, hivyo watakua wakiendesha timu zote mbili Fountain Gate FC na Singida Fountain Gate FC wakiwa wamiliki halali. 

Makau amesema timu ya Singida Fountain Gate itaendelea kuwepo Singida kutokana na makubaliano yao na wauzaji wa timu hiyo.

 Kwasasa Fountain Gate ina timu tatu za mpira wa miguu moja ikiwa ni timu ya wanawake ambayo inashiriki ligi kuu ya wanawake Tanzania, timu ya mpira wa miguu kwa wanaume Fountain Gate FC ambayo inashiriki Championship na hii ya sasa Singida Fountain Gate inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara (NBC).

By Jamhuri