Afisa Tarafa (Gavana) wa Tarafa ya Katerero iliyopo Bukoba mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku leo Jumatano Juni 05, 2024 akiambatana na Diwani wa Kata ya Bujugo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Vijijini Mhe. Privatus Mwoleka, Katibu wa CCM wa Kata Mama Byera, Mtendaji wa Kata Ndugu Barongo na Viongozi wengine wa Vijiji na Vitongoji, ametembelea kukagua na kujionea ujenzi wa Bweni la Wasichana kwenye Shule ya Sekondari Bujugo linalojengwa kupitia nguvu ya Ofisi ya Mbunge wa Bukoba Vijijini Dkt. Jasson Rweikiza, wadau mbalimbali na nguvu za wananchi.

Akiwa hapo amepata taarifa ya mradi huo utakaogharimu zaidi ya milioni 100 huku zaidi ya milioni 30 zilizochangwa na Ofisi ya Mbunge, wadau na wananchi zikiwa zimeshatumika huku ujenzi ukiwa umefika hatua ya level ya madirisha ambapo Gavana Bwanku ameamua kuunga mkono juhudi za Ofisi ya Mbunge Rweikiza, wadau na wananchi kwa kuchangia mifuko saba ya sementi.

Bweni hilo likikamilika litachukua takribani wanafunzi 80 na kusaidia pakubwa taaluma kwenye shule hiyo ambayo imekua ikifanya vizuri sana.