Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Kagera

Washuhudia Wataalamu wakubwa, mitambo mikubwa na wafanyakazi wakiwa site. Bandari ya Kemondo kufungua uchumi mzima wa mkoa.

Bandari ya Kemondo iliyopo kwenye Tarafa ya Katerero wilayani Bukoba- Kagera ni moja ya Bandari kubwa 10 Tanzania na ni Bandari yenye eneo kubwa sana nchini. Jana Alhamisi Mei 30, 2024 Afisa Tarafa wa Katerero mkoani Kagera Ndugu Bwanku M Bwanku amefika kutembelea mradi huo mkubwa wa upanuzi wa Bandari ya Kemondo unaogharimu Bilioni 20.

Kwenye ziara hiyo ya kujionea Jinsi Serikali ya Rais Samia ilivyowekeza upanuzi mkubwa wa Bandari hiyo, Gavana Bwanku aliongozana na Katibu wa CCM Kata ya Kemondo Ndugu Hamza Mzinga, Mtendaji wa Kata ya Kemondo Ndugu Cyriacus Sosthenes, Katibu wa Wazazi Kemondo Ndugu Zephlin Joseph, Mwenyekiti wa Kijiji cha Rwagati Ndugu Yahya Nuru na Mtendaji wa Kijiji cha Rwagati Ndugu Buruhani Mohamed huku wakiongozwa na Engineer wa Site Bandarini hapo Ndugu Josephat Robert na Meneja wa Usalama na Mazingira Ndugu Alex Ngasi.

Serikali ya Rais Samia imetoa Bilioni 20 kufanya upanuzi mkubwa wa Bandari hiyo ya Kemondo ili kuwezesha meli kubwa zaidi kama MV Mwanza kufika huku mitambo mikubwa na wafanyakazi zaidi ya 150 wakiwa site kila siku. Mradi umetoa ajira zaidi ya 150 kwa Vijana ukiwa umefikia 78.6% na utainua uchumi mkubwa wa mkoa mzima kwa kusafirisha mizigo yote ya Kanda ya Ziwa na abiria. Kazi Inaendelea chini ya Mkandarasi wa kampuni ya China Railway Major Bridge Engineering Limited (CRMBEG).