Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia,Dar

Kampuni ya simu ya Halotel na wafanyakazi wake leo wameshiriki katika zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kusheherekea na kuadhimisha miaka 7 ya kampuni na utoaji wa huduma za mawasiliano.

Zoezi la kuchangia damu ni majawapo ya taratibu ambazo Kampuni hiyo imejiwekea kama msaada wa kurudisha shukrani kwa jamii pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au vituo vya kutolea huduma za afya.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo katika ofisi za makao makuu ya Halotel, Mkuu wa kitengo cha Bidhaa na Mawasiliano Halotel, Sakina Makabu amesema kuwa katika kuhakikisha tunasaidia sekta hii ya afya nchini, tumeona ni vyema kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watanzania wenye uhitaji hasa wa damu kwenye hospitali mbalimbali nchini.

“Takwimu kupitia wizara ya afya nchini zinaonesha kwamba, uhitaji wa damu ni mkubwa sana kwa kuwa damu inahitajika sana na mama wajawazito, watoto, watu waliopata ajali pamoja na wanaofanyiwa upasuaji”, hivyo sisi kama Halotel kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) tumeendeleza zoezi hili la kushiriki na kuchangia damu kama hitaji maalum na ishara ya upendo kwa vitendo kwa watanzania ambao pia ndio wateja wetu”. Alisema Sakina.

Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Mawasiliano Halotel Sakina Makabu akiongea na waandishi wa Habari leo katika Ofisi za makao Makuu Halotel wakati wa zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Kampuni ya simu ya Halotel pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ikiwa ni moja ya msaada wa kurudisha shukrani kwa jamii katika kuelekea kilele cha kuadhimisha na kusherehekea miaka saba ya kutoa Huduma za mawasiliano hapana nchini pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au vituo vya kutolea huduma za afya.

“Tunatambua changamoto mbalimbali zinazoikumba sekta ya afya hasa katika upande wa uhitaji na upatikanaji wa damu katika hospitali na vituo vya afya kwa wagonjwa na kuamua kuendelea kuunga mkono juhudi za utatuzi wa changamoto hii kwa kujali na kutambua umuhimu kama kampuni na wafanyakazi tumeamua kurudisha upendo huu kwa jamii. ameongeza Sakina”

Akiongea wakati wa zoezi hilo la uchangiaji damu mmoja kati ya wafanyakazi waliochangia damu Bw;Dalili Musa amesema, “Tunajisikia furaha sana kushiriki katika zoezi hili moja kwa moja kwasababu huduma hii tuliyoifanya hapa kinaweza kuonekana ni kidogo ila kinaenda kuokoa maisha ya watu na hakika ni kitendo cha kuonesha upendo na kinaleta faraja Sana.

Kwa upande wa Uongozi wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa, Daktari wa dawa za usingizi katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), Juma Said Kabelele amesema “ Tumefarijika sana kwa kuja hapa na kufanya zoezi hili la kutoa damu na kampuni ya Mawasiliano ya Halotel na wafanyakazi wake, tunawashukuru sana kwa kuthamini afya za wananchi lakini pia kwa kuunga mkono jitihada za kuisaidia sekta ya afya nchini. Hii ni hatua kubwa na endelevu kwetu sisi katika kuimarisha ushirikiano wetu na Halotel kwa kiwango cha juu hasa katika kuboresha sekta ya afya kwa ujumla”.

Meneja wa huduma za Kidigitali Halotel Caroline Majaliwa akishiriki katika zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Kampuni ya simu ya Halotel pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)

“Tunapenda kutoa rai kwa watu binafsi, makampuni na Taasisi mbalimbali kuweza kujitoa na kushiriki zaidi katika zoezi la uchangiaji damu popote walipo nchini ili kuendelea kuipa ushirikiano sekta ya afya nchini katika kukabiliana na tatizo la upungufu wa damu katika benki ya taifa ya damu na hospitali mbalimbali maan mahitaji ni makubwa sana na kila iku kuna idai kubwa ya wagonjwa wanaohitaji huduma ya kuongezewa damu kulingana na tatizo husika la afya, hivyo utaweza kuokoa Maisha ya watanzania wengi kwa Pamoja.” ameongeza Mvungi.

Licha ya kampuni ya simu ya Halotel kupiga hatua kubwa katika kusambaza huduma za mawasiliano na intaneti yenye kasi na ubora wa hali ya juu ya 4G maeneo mengi nchini, kampuni hii imekuwa ikijihusisha na kutoa misaada mbalimbali kwa jamii ya watanzania.

Hii ni katika kuonesha jinsi inavyothamini na kujali jamii ya watanzania kwa nyanja mbalimbali, ikiwemo kuboresha sekta ya afya na zinginezo kama moja ya kipaumbele cha kampuni ya hii kwa maendeleo ya watanzania na nchi kwa ujumla.

Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu Halotel Bw: Thang Bui Van akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo katika ofisi za Makao Makuu ya Halotel leo katika zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Kampuni hiyo pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) ikiwa ni moja ya msaada wa kurudisha shukrani kwa jamii katika kuelekea kilele cha kuadhimisha na kusherehekea miaka saba (07) ya kutoa Huduma za mawasiliano hapana nchini pamoja na kuunga mkono jitihada za serikali kupitia Sekta ya Afya katika kukabiliana na changamoto ya uhaba wa damu katika hospitali au vituo vya kutolea huduma za afya.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya Halotel Bw: Dalili Musa Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (wa kwanza Kushoto) na Bw; Pius Joseph Tibasiga Afisa Manunuzi Halotel ( Wa pili kushoto) wakishiriki katika zoezi la uchangiaji damu lililoendeshwa na Kampuni ya simu ya Halotel pamoja na Wafanyakazi kwa kushirikiana na Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI)

By Jamhuri