KIUNGO na Nahodha wa Timu ya Taifa ya Croatia, Luka Modric ameibuka mshindi wa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 na kupewa Mpira wa Dhahabu wakati timu yake ikipoteza mchezo wao wa fainali kwa kukubali kichapo cha bao 4-2 kutoka kwa Ufaransa huko Urusi.

 

Modric ambaye amemaliza mashindano akiwa na mabao mawili, ameisaidia timu yake kutinga fainali ikiwa ni mara ya kwanza kwa timu hiyo kufikia hatua hiyio kubwa ya kihistoria.

 

Staa huyo wa Real Madrid ameonyesha kumvutia zaidi uchezaji wake, Rais wa Croatia, mwanamama Kolinda Grabar-Kitarovic wakati wa kukabidhiwa zawadi hiyo na Rais wa FIFA, Gianni Infantino na Rais wa Urusi, Vladimir Putin wakati hafla za kukabidhi ubingwa huo.

 

Modric amewashukuru mashabiki wa Croatia na wachezaji wenzake kwa sapoti kubwa waliowapa hadi kufikia fainali licha ya kufungwa.

Mbelgiji, Eden Hazard akiwa mchezaji Bora wa Pili na kutunukiwa mpira wa Silver, na Mfaransa, Antoine Griezmann akiibuka mchezaji Bora wa Tatu na kupewa mpira wa shaba.

 

Kinda Mfaransa mwenye umri wa miaka 19, Kylian Mbappe ameibuka mchezaji Bora Mwenye Umri mdogo zaidi, akifunga mabao manne kwenye mashindano hayo.

Kipa wa Ubelgiji, Thibaut Courtois amechukua Medani ya Dhahabu kwa kuwa kipa Bora wa mashindano akiisaidia timu yake kushika nafasi ya tatu huku akiruhusu mabao sita pekee kwenye mechi saba na clean sheets tatu.

Nahodha wa Uingereza,  Harry Kane ameibuyka na kiatu cha dhahabu kwa kuwa mfungaji bora akiwa na jumla ya mabao sita, Griezmann manne, na kuwa wa pili akichukua kiatu cha Silver na Mbelgiji Romelu Lukaku, wa tatu akichukua kiatu cha shaba.

Mbappe, Cristiano Ronaldo na Denis Cheryshev pia wana mabao manne kila mmoja lakini wameshindwa kwenye kipengele cha assists kwani wana assists chache. Grizemann.

Fifa imeitangaza Timu ya Taifa ya Hispania ndiyo timu yenye nidhamu zaidi kwani imemaliza mashindano ikiwa na kadi mbili za njano pekee.

Please follow and like us:
Pin Share