Na Mandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila leo Novemba 28, amekabidhi magari matatu ya kisasa ya wagonjwa katika Hospitali za Rufaa za Mkoa huo ikiwemo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala-Wilaya ya Kinondoni, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Temeke, na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana- Wilaya ya Ilala

Akikabidhi Magari hayo ya kisasa ya kubebea wagonjwa RC Chalamila amemshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya na anaendelea kufanya katika sekta ya Afya na Sekta nyingine hapa nchini.

Vilevile amewataka waganga wakuu wa hospitali ambazo zimekabidhiwa magari hayo kuyatunza ili yaweze kutoa huduma kwa muda mrefu.

Aidha naye Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Amana Dkt Kiwelu amesema magari hayo yanakwenda kurahisisha utoaji wa huduma za Afya kwa jamii zilizo bora na kwa haraka zaidi kwa kuwa ni magari ya kisasa yana vitu vyote muhimu ” Yaan ni ICU inayotembea Alisema Dkt Kiwelu