Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke inapanga kufanya maboresho makubwa ya miundombinu kwa kurekebisha jengo la bima na kujenga gorofa nne hadi sita. Lengo ni kuboresha huduma kwa wananchi. Hatua hii imethibitishwa katika kikao kazi cha timu ya uendeshaji kilichofanyika leo hospitalini.
Uongozi wa hospitali uliona mpangilio wa usanifu wa 3D wa miundombinu mpya, ikiwa ni pamoja na jengo jipya la Bima na mpangilio wa wodi na vyumba vya kuona wagonjwa.
Mganga Mfawidhi, Dkt. Joseph Kimaro ameonyesha furaha yake na matarajio ya muonekano mpya wa hospitali, akisema kuwa maboresho haya yataongeza uwezo wa kutoa huduma bora.
Mpango wa ujenzi uliwasilishwa na timu ya waandisi kutoka Taasisi ya Mifupa (MOI), ikiongozwa na Mhandisi Paul Korosso. Mhandisi huyo amesisitiza umuhimu wa mpango kazi wakati wa ujenzi au ukarabati.
Hospitali inaendelea kuweka mkazo katika kuboresha huduma, na ujenzi huu unalenga kuboresha sana muonekano na utoaji wa huduma za afya kwa jamii.