Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea na hatua za kuimarisha sekta ya bandari kwa ujenzi wa maeneo mbalimbali ikiwemo ujenzi wa bandari jumuishi Mangapwani, bandari ya Shumba na Mkoani ili kuleta ufanisi wa sekta hiyo.

Rais wa Dkt.Mwinyi amesema hayo katika hafla fupi ya uzinduzi wa bandari ya Fumba Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 08 Januari 2024 katika shamrashamra za Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa bandari za kusafirisha abiria zitaimarishwa na nyingine mpya kujengwa ikiwemo.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesema tatizo la kuchelewa makontena kutoka Mombasa limepata ufumbuzi kwa bandari mpya ya Fumba.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amesema ufanisi wa bandari ukiongezeka bei za bidhaa mbalimbali zitashuka nchini.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewapongeza kampuni ya Fumba Inland Container Terminal kwa kuwekeza shilingi bilioni 15.3 katika bandari ya Fumba ambayo itakuwa na uwezo wa kuchukua nafasi ya makontena zaidi ya 3,000.

By Jamhuri