Makamu wa Pili wa Rais amewataka wananchi kuyalinda na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu Z’Bar

Makamu wa Pili wa Rais Hemed Suleiman Abdullah amewataka wananchi kuendelea kuyalinda na kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa Kuunga Mkono jitihada za Serikali katika kuleta Maendeleo Nchini.

Hemed ameyasema hayo katika hafla ya uwekaji wa jiwe la Msingi Skuli ya Kiwani Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba ikiwa ni katika muendelezo wa Shamrashamra za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema ili kuyaenzi Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kunahaja ya kuwafahamisha Vijana maana halisi ya Mapinduzi hayo kupitia kasi ya Maendeleo Nchini.

Aidha Mhe. Hemed amesema Ujenzi wa Jengo la ghorofa Kiwani lenye madarasa 45 linafanya kua ni Skuli pekee yenye idadi kubwa ya madarasa Kisiwani Pemba.

Amesema Jengo hilo pamoja na Majengo mengine mapya yatawekewa vifaa vipya ili Wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.

Mhe. Makamu wa Pili wa Rais amewataka Wananchi kulinda rasilimali na miundo mbinu ili iweze kutumika kwa muda mrefu.

Nae Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohamed Mussa amesema Kuongezeka kwa miundombinu kumepelekea matokeo Bora ambapo Wilaya ya Mkoani imeibuka ya kwanza Kitaifa.

Aidha Mhe. Lela amempongeza Raisi wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwa Kasi ya maendeeo na Kuifanya Sekta ya Elimu kua moja kati ya Vipaumbele katika Maendeleo.

Kwaupande wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Matter Zahor Massoud ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuboresha miundombinu ya Elimu katika Mkoa wake.

Mhe. Mattar amesema ili manbadiliko yakimaendeleo yaweze kufikiwa nilazima kuipa kipaumbele sekta ya Elimu.

Akiwasilisha taarifa ya Kitaalamu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bw. Khamis Abdullah Said Ujenzi wa Skuki ya Kiwani utagharibu Tsh. 6.2 hadi kukamilika kwake.

Aidha amesema Ujenzi huo ulianza Mwezi May mwaka 2023 na unatarajiwa kukamilika mwanzoni mwaka huu wa 2024.