Na Mary Margwe, JamhuriMedia,Hanang

Idadi ya vifo vya waliopoteza maisha katika maafa ya maporomoko ya udongo huko Wilayani Hanang mkoani Manyara vimefikia 63, ambapo Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ameongeza kuaga miili wilayani Hanang mkoani Manyara.

Waziri Majaliwa amesema jumla ya vifo ni 63 kati yao wakiwemo wanawake 40, na wanaume 23, kati ya hao watu wazima ni kuanzia miaka 18 na kuendelea ni 40 ambapo kati yao wanawake ni 26 na wanaume hi 14.

“Ndugu Watanzania katika maafa haya yaliyotokea Novemba 3 tumepoteza ndugu zetu wapatao 63, kati yao wakiwemo wanawake 40, na Wanaume 23, kati ya hao wat wazima ni kuanzia miaka 18 na kuendelea ni 40 ambapo kati yao wanawake ni 26 na Wanaume hi 14, huku watoto chini ya miaka 18 wakiwa 23 kati yao wanawake ni 14 na Wanaume ni 9 na kufanya jumla ya watu 63” alisema Waziri Mkuu.

Aidha Waziri Mkuu amesema katika tukio hilo pia kuna majeruhi wapatao 116 kati yao wanawake ni 60 na wanaume 56, kati yao watu wazima ni 60 wakiwemo wanawake 31 na wanaume 29, huku watoto chini ya miaka 18 wakiwa ni 66 wanawake ni 29 na wanaume 27.

“Ndugu Watanzania nninmaafa makubwa sana sana ambapo pia katika maafa haya tumepata uhalibifu wa nyumbaza kuishi, mashamba, mitambo mbalimbali ya magari, na tumepita kwenye maeneo yaliyoathirika, binafsi nimepata bahati ya kufika katika Kijiji Cha Gendabi nyuma ya mlima kule, kile Kijiji sasa kimeachwa nyumba za upande wa kulia na kushoto tu, katikati nyumba zote zimeondoka limebakia kanisa tu” amefafanua Waziri Mkuu.

Aidha kufuatia hilo Waziri Mkuu amesema Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maelekezo kuwa huduma zote za miili zimefanywa na Serikali ikiwemo kununua majeneza na kusafirishwa kwa miili yote hadi majumbani kwao kwaa ajili ya taratibu zingine za kidini ama kimila ziweze kuendelea.

Amesema wale waliopata majerugi pia Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza kwa kuwa matibabu ni gharama hivyo matibabu kwa majeruhi wote yatatolewa bure hadi hapo afya zao zitakapokua zimetengemaa uzima.

” Majeruhi wote ambao nyumba zao zimetoweka kabisa wataishi kwenye makambi ambapo tayari kambi tatu zipo kwenye shule tatu za makambi maalum na wakiwa hapo watakua wakipatiwa huduma za maji, chakula, na matibabu kama kuna matatizo ya kiafya, na tunawashukuru sana wale wote waliowapokea waanga kwa ajili ya kuwasaidia waanga na kuwapa hudumaza waliokosa sehemu za kuishi, huku Serikali ikiendelea kupitia kutambua wangapi na wako wapi na athari ni zipi, ambapo Rais Samia ameagiza kufanya tathimini ya madhara haya” amesema Waziri Mkuu.

Aidha amefafanua kufuatia maelekezo hayo taasisi zote za Serikali tayari zipo hapo Katesh Ofisi wpya Waziri Mkuu kitengo cha maafa pia kipo hapo kwa ajili ya kushirikiana na Kamati ya Maafa ya Mkoa wa Manyara pamoja na kamati ya maafa ya Wilaya ya Hanang ikiongozwa na mkuu wa wilaya hiyo.

“Wizara zote ambazo zinaguswa na uharibifu huu zote ziko hapa ,Wizara ya afya wapo hapa na Ummy Mwalimu yuko hapa pamoja na madaktari bingwa wa mifupa wote wako hapakwaajilinya kutoa huduma, Wizara ya mambo ya ndani, Uhamiaji, Zimamoto wote wako hapa kuhakikisha mambonyote yanaenda sawa na Usalama unakua mzuri katika maeneo haya” amesema Waziri Mkuu.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema bado Serikali inaendelea kufuatilia na kutafiti kilichosababisha kutokea Kwa maporomoko ya udongo, hivyo Wizara ya Madini chini ya Waziri wake Peter Anthony Mavunde yuko hapo pamoja na wataalam wa miamba kuona nini kilichosababisha kutokea Kwa tukio hilo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua meneo yaliyoathika kwa mafuriko katika kijiji cha Gendabi wilayani Hanang, Disemba 4, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)