Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Camillus Wambura amesema nishani zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zitaleta ari ya uwajibikaji kwa Maafisa, Wakaguzi na Askari wa Jeshi la Polisi kwa kutekeleza majukumu ya ulinzi na usalama kwa bidii na kuleta tija kwa Taifa.

Akiwavisha nishani Maafisa, Wakaguzi na Askari 45 kwa niaba ya Askari 677 wa Kamisheni ya Polisi Zanzibar ambao wametunukiwa nishani hizo, kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu MHE. DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, IGP WAMBURA amewahimiza Waliopata na wasiopata nishani kufanyakazi kwa uaminifu na Uadilifu.

Nae Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi MHE. IDRISA MUSTAFA KITWANA amesifu utendaji wa Jeshi la Polisi Mikoa ya Zanzibar na kueleza kuwa, Nishani walizopewa ni kielelezo cha Utendaji mzuri.

By Jamhuri