SEOUL, KOREA: Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo mkoani Dodoma.

Kabla ya uteuzi huu Prof. Makubi alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dk. Alphonce Biola Chandika ambaye amemaliza muda wake.