Na Isri Mohamed

Ule msemo wa ikisikika nyuma geuka wa mwisho anakuwa wa kwanza umejidhihirisha wazi kwa timu ya taifa ya Ivory Coast ambayo licha ya kufuzu hatua ya 16 bora kwa njia ya ‘Best Looser’ lakini wametwaa ubingwa wa AFCON 2023 kwa kuifunga Nigeria mabao mawili kwa moja.

Katika fainali iliyochezwa usiku wa kuamkia leo Januari 12, Nigeria walitangulia kupata bao kupitia kwa Nahodha wao, William Ekong dakika ya 38, lililowavuruga Ivory Coast na kuanza kucheza kwa presha mpaka dakika ya 72 waliposawazisha kupitia kwa Franck Kessie na baadae dakika za jioni Sebastien Haller akafunga bao la ushindi lililowapa ubingwa.

Hii ni mara ya tatu kwa Ivory Coast kutwaa ubingwa huo huku wakiingia kwenye rekodi ya nchi 12 pekee zilizowahi kuandaa michuano hiyo na kuchukua ubingwa, ambapo kwa mara ya kwanza Misri waliweka rekodi hiyo mwaka 2006.

Katika michuano hiyo pia kocha wa Ivory Coast, Emmerse Fae ameshinda tuzo ya kocha bora wa michuano, huku bwana mdogo Simon Adingra mwenye umri wa miaka 22 akichukua tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa Afcon kwa kuwa mchezaji wa kwanza kutoa pasi mbili za magoli ‘Assist’ kwenye mchezo wa fainali kwa karne hii ya 21.

By Jamhuri