Na Isri Mohamed

Mchezaji wa klabu ya Spartak Moscow ya nchini Urusi, Quincy Promes mwenye umri wa miaka 32, amehukumiwa kwenda jela miaka 6 baada ya kukutwa na hatia ya kuuza dawa za kulevya.

Promes ambaye amewahi kuzitumikia klabu za Ajax Amsterdam, FC Seville na timu ya Taifa ya Uholanzi mwaka 2014-2021 hakuwepo wakati hukumu inatolewa katika mji wa Amsterdam Uholanzi.

Katika kesi nyingine, Promes amehukumiwa kifungo cha miaka 18 kwa kumpiga na chuma kwenye magoti binamu yake, kosa alilolitenda mwaka 2020.

Baada ya hukumu, Quincy Promes hajaridhishwa na uamuzi wa mahakama hivyo anakwenda kukata rufaa.

By Jamhuri