Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar

Winga wa zamani wa Yanga Raia wa Congo, Jesus Moloko amejiunga na klabu ya AL Sadaqa Benghazi inayoshiriki ligi kuu ya Libya.

Moloko ambaye alitemwa na Yanga ili kupisha usajili wa Agustine Okrah Amejiunga na klabu hiyo ambaye kwenye msimamo wa ligi kuu Libya inashika nafasi ya nane baada ya kucheza michezo tisa ikiwa na pointi sita pekee.

Kupitia Ukurasa wao wa Instagram wa Klabu hiyo wameposti picha ya Moloko na kuandika ujumbe huu.

“Kabla ya dirisha la usajili kufungwa Winga Mkongomani Jesus Moloko Atakuwa sehemu ya Ngome Yetu akitokea Yanga ya Tanzania”

Kabla ya kutangazwa kujiunga na Klabu hiyo Moloko alikuwa akihusishwa na Matajiri wa Dhahabu Geita Gold, Ambao Licha ya Juhudi Kubwa Walizofanya ili Kunasa Saini yake Lakini Hazikuzaa Matunda.