Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi -Simiyu

Jeshi la Polisi Mkoani Simiyu limewahimiza wanachi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vya ukatili Mkoani humo vinavyofanywa na Baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu.

Kauli hiyo imetolewa leo Agasti 27,2023 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna msaidizi wa Polisi ACP Edith Swebe wakati wa sherehe za mavuno katika Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania KKKT Ushirika wa Tumaini Bariadi alipopata nafasi ya kutoa elimu ya Ukatili wa kijinsia.

ACP Swebe ameongeza kuwa viongozi wa dini wanapaswa kutumia nyumba za ibada kukemea vitendo viovu pamoja na kukemea vitendo vya ukatili wa kijinsia unafanywa na baadhi ya watu wasio na hofu ya Mungu.

Amewaomba wazazi kuongeza ulinzi kwa watoto ambapo amebainisha kuwa kundi hilo kwa sasa ukiangalia takwimu ndio waathirika wa kubwa dhidi ya vitendo vya ukatili huku akiwaomba kutoa taarifa hizo kwa vyombo husika.

Pia kamanda swebe amesema vitendo vya ukatili vinarudisha Nyuma maendeleo kwa makundi yote yanayofanyiwa ukatili katika jamii.

Sambamba na hilo amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi hilo ikiwa ni pamoja na kuiombea Nchi na Mkoa wa Simiyu ili kuendelea kuwa shwari.