KATIBU WA UWT JUDITH LAIZER KUTATUA TATIZO LA VYOO KATIKA SHULE YA YA MSINGI ILULA NA ISOLIWAYA ZILIZOPO KILOLO

Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiongea na baadhi ya viongozi ,walimu na wanafunzi wa shule ya msingi Isoliwaya wakatika wa kukabidhi msaada huo kwa ajili ya kujengea vyoo ya walimu wa shule hiyo
Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer akiwa ameambatana na baadhi ya viongozi wa chama hicho Leah Moto na Nancy Nyalusi walikuwa kwenye ziara ya kusherekea miaka 41 ya chama cha mapinduzi 
Hili ni moja ya jengo lashule ya msingi Ilula iliyopo katika tarafa ya mazombe wilayani kilolo mkoani Iringa 
Baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi wilaya ya kilolo wakiwa katika kusherekea miaka 41 ya kuzaliwa chama chao kwa kufanya shughuli za kijamiii
 
WALIMU wa shule ya msingi Ilula na Isoliwaya zilizoko katika kata ya Ilula Wilaya ya Kilolo wanakabiriwa na magonjwa ya Mlipuko kwa kukabiliwa na changomoto ya choo.
Shule hizo zilizotenganishwa baada idadi kubwa ya wanafunzi, walimu 49 wanalazimika kutumia choo Chenye matundu mawili hali inayohatarisha usalama wa afya zao.
Akizungumza mbele ya Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer, mwalimu Msaidizi wa shule ya Msingi Isoliwaya, Huruma Mbena alisema hali hiyo inahatarisha afya za walimu kutokana na changamoto hiyo.
Mbena alisema kuwa baada ya shule hizo kutenganishwa vyoo vya walimu vilibaki kwa shule ya Ilula hivyo kutokana na idadi kubwa ya walimu wanalazimika kutumia vyoo hivyo licha ya kutotosheleza kutokana na idadi kubwa ya walimu.
Aidha alisema kuwa shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya nyumba za walimu ambao hadi sasa walimu 21 wanaishi katika nyumba za kupanga hali inayowaletea ugumu wa maisha zaidi.Alisema kuwa changamoto nyingine wanayokabiliana nayo ni ukosefu wa ofisi za walimu na ofisi ya mwalimu mkuu na kulazimika kutumia moja ya darasa kama ofisi na kupunguza idadi ya madarasa.
Akijibia hoja zilizopo kwenye risala Katibu wa umoja wa wanawake wa Ccm (UWT) wilaya ya Kilolo Judith Laizer alisema kuwa umoja huo umewaleta mifuko ya saruji kumi na tano (15) na bati saba kwa ajili ya kusaidia kujenga vyoo vya walimu ili kupunguza adhabu wanayoipata.
“Kweli ukikosa huduma ya choo bora walimu hawezi kuwa huru kufundisha wanafunzi maana anaenda chooni huku akijua kuwa wanafunzi wake wanamtazama kwa mtazamo tofauti na ukizingatia maisha ambayo wanaishi majumbani kwao” alisema Laizer
Laizer alisema kuwa changamoto nyingine kama ukosefu wa nyumba za walimu,upungufu wa vyumba nane vya madarasa na ukosefu wa ofisi ya walimu atazifikisha kwa viongozi wa wilaya na kwa mbunge wa jimbo hilo Vennace Mwamoto.
“Hizi changamoto zenu zinatatulika kwa kuzingatia kuwa vingozi wa wilaya hii ni wachapakazi na waadilifu kuwatumikia wananchi nauhakika kuwa watakuja hapa na kuzitafutia ufumbuzi hizi changamoto kwa kuwa nitazifikisha kama nilivyozichukua hapa” akisema Laizer
Lakini Laizer aliwataka viongozi wa bodi ya shule hilyo kuhakikisha kuwa wanafanya kazi kwa ukaribu na wazazi wa shule hiyo kwa kuhakikisha wanaanza ujenzi wa nyumba za walimu pamoja na kujenga vyumba vya madarasa na mwishoni mbunge na halmshauri watamalizia sehemu iliyobaki.
“Naombeni nyie viongozi kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi hao bila kuwashirikisha walimu kwa kuwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli kama alivyoagiza kuwa elimu bure bila malipo” alisema Laizer
Laizer aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa kufanya kazi kubwa ya kufaulisha kwa wastani unaolidhisha na kuwaomba kuongeza bidii kufundisha huku wakibuni mbinu mpya za ufundishaji.