Kiingereza cha mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku maarufuku ‘Msukuma’ kimezua gumzo mitandaoni baada ya mbunge huyo kumuuliza swali mgombea wa ubunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (Eala), Habid Mnyaa.

Gumzo hizo zimeanzia bungeni baada ya kupewa nafasi ya kuuliza swali ambalo aliliuliza kwa lugha ya kiingereza katika kikao cha Bunge leo Septemba 22,2022 ambalo mgombea alishindwa kuelewa na Spika akamtaka Msukuma kurudia tena swali lake.

Gumzo hizo zimetokana na Musukuma kutajwa kuwa elimu yake ni ya darasa la saba.

Msukuma alipewa nafasi ya kuuliza swali na Spika Dkt. Tulia Ackson baada ya mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka kumaliza kuuliza maswali na ndipo shangwe zilipoanzia bungeni.