Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson leo Septemba 22,2022 amewatangaza washindi tisa walioibuka na ushindi kwenye uchaguzi wa wabunge wa Afrika Mashariki (EALA), kati ya wagombea 20 uliofanyika bungeni, jijini Dodoma

Akitangaza Majina ya Washindi hao Spika Dkt Tulia amewataka Wabunge hao kwenda kuliwakilisha vyema Taifa katika Bunge la Afrika Mashariki kama ambavyo wameahidi kwenye Kampeni zao
Washindi hao ni.
1;Angella Kizigha(CCM)
2;Nadra Mohammed(CCM)
3;Dkt Shogo Richard Mlozi(CCM)
4 ;Abdulla Hasnuu Makame(CCM)
5. Machano Alli Machano(CCM)
6.Mashaka Khalfan Ngole(CUF)
7.Ansari Abubakar Kachwamba(CCM)
8. James Kinyasi Millya(CCM)
9.Dkt. Ng’waru Jumanne Magembe(CCM).