Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana ameongoza Ujumbe wa CCM kwenye mazungumzo na Vo Van Thuong, Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam, Jijini Ha Noi, Viet Nam.

Katika mazungumzo hayo, Kinana aliwasilisha ujumbe maalum kutoka kwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, wa kuhimiza ushirikiano wa kiuchumi baina ya nchiĀ  hizo mbili ili kuwanufaisha wananchi wa Tanzania na Vietnam.

By Jamhuri