Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia

Watu wanne wamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu katika kijiji cha Buchurago kata ya Bugorora wilayani Missenyi mkoani Kagera huku wengine wanne wakilazwa katika Hosptali ya St.Tereza.

Mkuu wa Mkoa Kagera, Fatma Mwassa amesema serikali inaendelea na uchunguzi kwa watu wote walio tengamana na wagonjwa na tayari serikali nimechukua sampuli 18 kutokana na ugonjwa huo uliotokea Novemba 29, 2023.

“Tumebaini kuna ugonjwa wa kipindupindu tayari tumefanya uchunguzi na kubaini ugonjwa huo tunatoa wito kwa wananchi wetu kuendelea kuchukua tahadhari ,kwa sababu huu ugonjwa ni hatari sana ,tumechukua hatua na tunaendelea kuwabaini wananchi waliokutana na wagonjwa awali ili kuona kama kuna dalili za kupata ugonjwa huo.”alisema Mwassa

Alisema ugonjwa huo ni hatari na inatakiwa kuendelea kuchukua tahadhari maana unaenea kwa kasi. Katika hatua nyingine amewataka wakazi wa mkoa huo kuacha mikusanyiko,kula chakula kwenye mikusanyiko na kunawa mikono mara kwa mara ili kupunguza madhara yanatoweza kujitokeza.