Na Mwandishi wetu,JamhuriMedia,Simaniiro

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Manyara, Kiria Ormemei Kurian Laizer amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Simaniiro.

Msimamizi wa uchaguzi huo ambalo umefanyika jana Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Sizaria Makota ametangaza matokeo hayo kuwa Kiria amepata kura 315.

Amesema Anna Shinini ameshika nafasi ya pili kwa kupata kura 205 na Haiyo Mamasita kawa watatu kwa kupata kura 34.

Makota amesema jumla ya kura zilikuwa 560, kura zilizoharibika ni sita na kura halali 554.

Akizungumza baada ya kutangazwa kushika nafasi hiyo Laizer amesema atahakikisha Simanjiro inakuwa moja kwa kuvunja makundi.

“Kipaumbele changu itakuwa siasa ya uchumi na kuhakikisha tunapiga hatua wote kwa pamoja,” amesema Laizer.

Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka amesema hivi sasa Kiria ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro hivyo makundi yamevunjwa.

Kwa upande wa katibu wa siasa na uenezi Kiria amemtangaza Mosses Makeseni kwa kupata kura 61 kwa kuwabwaga Papai Njiday kura 25 na Mterian Laizer kura tatu.

By Jamhuri