Na Mwandishi Wetu JAMHURI MEDIA Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande amesema kwa sasa Tanzania kiwango chaupatikanaji wa chakula kimeongezeka na hali ya umaskini wa chakula imepungua.


Amesema ahueni hiyo ni kutokana na mchango wa Benki ya Dunia katika kufadhili tafiti zilizofanyika nchini kwa kipindi cha miaka 15 kuanzia 2008 ikiwa ni kubaini hali ya umasikini na mwenendo wa uaptikananji wa chakula na upunguzaji wa vifo vya mama na mototo.


Naibu Waziri Chande ameyasema hayo katika Kongamano la kujadili masuala mbalimbali yaliyojiri wakati wa utekelezaji wa tafiti zilizofadhiliwa chini ya mradi wa Benki ya Dunia uitwao ‘Living Standard Measurement Study-Intergrated survey on agriculture’ (LMS-ISA) leo Novemba 14, 2023 Jijini Dar Es Salaam.


“ Kiwango cha umasikini wa chakula kwa sasa hasa umaskini wa upatikanaji wa chakula, chakula kinapatikana kwa wingi na cha kutosha, ambacho sisi watanzania leo tunalisha hadi nchi jirani.”Amesema Naibu Waziri Chande.


Dkt Albina Chuwa ambaye ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali amesema utafiti huo umeleta mafanikio makubwa sana ndani ya bara la Africa, kufuatilia kaya moja hadi nyingine ambapo kaya hizo zilifatiliwa kwa kipindi cha miaka 15.


Dkt. Chuwa amesema utafiti huo umeiwezesha sana Serikali ya Tanzania katika kupunguza umasikini wa chakula uliokithiri huku kiwango hicho kikitarajiwa kushuka Zaidi kwa miaka ijayo.


“ Tumeona juzi vifo vya mama wajawazito vimepungua kwa kasi kubwa kutoka 530 mwaka 2015/2016 mpaka 104 kwa kila vizazi hali laki moja, vifo vya watoto wachanga, udumavu tumepunguza kutoka asilimia 34 mpaka 30” Amesema


Katika utafiti uliofanyika 2018 ulionyesha kuwa takribani asilimia 60 ya watanzania wanaishi maeneo ya vijijini na shughuli zao kuu ikiwa ni kilimo huku aslimia nane ya watanzania ndiyo wakiwa masikini.


Kutokana na majanga ya asili kama vile magonjwa mlipuko mafuriko na mabadiliko ya tabia nchi ambayo yamekuwa yakiathiri kilimo idadi kubwa wamekuwa wakizalisha chakula kisichokuwa na virutubisho vinavyohitajika kwa ajili ya matumizi yao na kusababisha matatizo ya kiafya ikiwemo udumavu kwa watoto.


Kwa upande wake Kamisaa wa Sensa Dkt.Anna Makinda ametoa wito kwa wataalamu wa Takwimu kuhakikisha taarifa zinawafikia wahusika waiofanyiwa utafiti na siyo kukaa nazo licha ya kwamba tafiti hizo zitakwenda kuibua mambo makubwa na yenye manufaa kwa nchi.


“Mara nyingi utafiti huu hauendi kwa watu wenyewe, Hawa wataalamu wa takweimu ni wakati umefika sasa utafiti wao uweze kuwatumikia wale watu waliohusika wenyewe na serikali na watawala wengine. Maana yake mara nyigi taarifa hizi zinakaa kwenye mashelfes zinabaika kwenye ofisi zao haziendi kwa wahusika na wanaopaswa kuzitumia hawazioni”amesema

Naye Gero Cerletero wa Banki ya Dunia amesema benki hiyo itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuwezesha ufanyaji wa tafiti ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na data muhimu zitakazosaidia katika utungaji wa sera na maendeleo.