Msanii Koffi Olomide maarufu Mopao anatarajia kufanya shoo katika ukumbi wa The Breez Complex ulioko Sabasaba barabara ya kuelekea Kiseke Jijini Mwanza.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Mratibu wa shoo ya Koffi Olomide Jijini hapa Victor, amesema msanii huyo anatarajia kufanya shoo yake wiki ijayo.

Amesema kuwa Koffi Olomide atafika Jijini Mwanza akiwa na Bendi yake kwaajili ya kuwapa burudani wakazi wa Mwanza na Mikoa jirani.

Niwaombe sana Wakazi wa Mikoa ya Kanda ya ziwa kujitokeza katika tamasha kubwa la msanii wa dansi ili muweze kushuhudia mambo makubwa anayoyafanya kwa upande wa viingilio tutawajulisha hivi karibuni hivyo kaeni mkao wa kula”,amesema Victor

Kwa upande wake Kiongozi kutoka The Breez Nashoni Msafiri, amesema wanatarajia kupokea ugeni mkubwa wa msanii Kofii Olomide ambae anakuja kutoa burudani kwa Mashabiki wake na wapenzi wa Muziki.

Mratibu wa shoo ya kofii Olomide Jijini Mwanza Victor akizungumza na waandishi wa habari leo hii juu ya ujio wa Msanii wa mziki wa dansi