Watanzania wamehamasika kushiriki Tamasha la JAMAFEST

Na Eleuteri Mangi,JamhuriMedia,Burundi

Balozi wa Tanzania nchini Burundi Dkt. Jilly Elibariki Maleko amesema Watanzania wamehamasika na wamekuja kwa wingi katika Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linalofanyika kuanzia Septemba 4-12, 2022 nchini Burundi.

Balozi Dkt. Jilly amesema hayo juzi mara baada ya kutembelea mabanda ya wajasiriamali kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki walioleta bidha zao kwenye hilo.

Nimemaliza kutembelea mabanda ya Tanzania na nchi nyingine, nimeona hamasha kubwa sana Watanzania waekuja kwa wingi, watu mbalimbali wameleta bidhaa za Sanaa, chakula na kwa sababu Burundi wanapenda sana bidhaa za chakula kutoka Tanzania. Nimeona jinsi wanavyochangamkia mchele, dagaa, viungo vya chakula, mafuta, nguo batiki, mapambo ya mwili na picha za Tingatinga, kwa kweli maonesho yamefanaā€¯ amesema Mhe. Balozi Dkt. Jilly.

Balozi wa Tanzania nchini Burundi Mhe. Dkt. Jilly Elibariki Maleko (aliyevaa miwani) akitembelea mabanda ya wajasiriamali ya Watanzania alipotembelea mabanda hayo wakati wa Tamasha la Tano la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST) linaloendelea nchini Burundi.

Balozi Dkt. Jilly ameongeza kuwa ofisi yake inashirikiana pamoja na watanzania ambao wamekuja kweny tamasha hilo kwa kuwahamasisha watu mbalimbali wakiwemo Wtanzania waishio nchini Burundi, jamii ya kimataifa wakiwemo Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao, wafanyakazi wa mashirika pamoja na kikanda na kuwahimiza kutembelea mabanda yote ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Pamoja na maonesho hayo ya Sanaa na Utamaduni, mada mbalimbali ziliwasilishwa tamasha hilo kiwemo jukumu la teknolojia ya kisasa kwa kutumia utamaduni, tasnia ya sanaa na utalii, ushiriki wa vijana katika shughuli za sanaa katika jumuiya ya EAC pamoja na matokeo ya uvumbuzi katika sanaa na utamaduni.