Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Rufiji

Serikali imezipongeza Kamati za Ulinzi na Usalama pamoja na Kamati za Maafa katika maeneo yote yaliyokumbwa na maafa ya mafuriko kwa namna wanavyosimamia zoezi la uokoaji na kuratibu kwa makini misaada inayotolewa kwa ajili ya waathirika.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo ametoa pongezi hizo wilayani Rufiji, wakati aliposhuhudia Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakar Kunenge akipokea msaada wa tani 20 za chakula na Mitungi ya Gesi na Majiko yake 300 iliyotolewa na Kampuni ya Lake Energies kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Rufiji waliokumbwa na mafuriko.

Dkt. Jafo amesema misaada hiyo ni kielelezo cha wadau na wawekezaji nchini kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye yeye mwenyewe Rais amekuwa kiongozi katika kuchangia misaada hiyo kwa ajili ya watanzania wa maeneo mbalimbali yaliyokumbwa na changamoto ya mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mungano na Mazingira Dkt. Selemani Jafo akijadiliana jambo na Mkuu wa kitengo cha Uhusiano wa Lake Energies, Stephen Mtemi(watatu toka kushoto)wakati aliposhuhudia Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakar Kunenge akipokea msaada wa tani 20 za chakula na Mitungi ya Gesi na Majiko yake 300 iliyotolewa na Kampuni ya Lake Energies kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Rufiji waliokumbwa na mafuriko.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakar Kunenge akipokea msaada wa tani 20 za chakula na Mitungi ya Gesi na Majiko yake 300 iliyotolewa na Kampuni ya Lake Energies na kukabidhiwa na Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Nassoro Abbakari(kushoto)kwa ajili ya wananchi wa wilaya ya Rufiji waliokumbwa na mafuriko.

By Jamhuri