Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini imepanga kutoa leseni 12,456 katika mwaka wa fedha 2024/25. Bunge limeelezwa.

Akiwasilisha bungeni leo Juni 4, 2024, Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025, Waziri wa Fedha Dk Mwigulu Nchemba amesema leseni hizo zinajumuisha leseni mpya 1,126.

“Katika mwaka 2024/25, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha imepanga kutoa leseni 12,456, ikijumuisha leseni mpya 1,126 na kuhuishwa leseni11,330; kufanya kaguzi 12 kwa kuzingatia vihatarishi katika michezo mbalimbali ya kubahatisha.

“Kutekeleza operesheni nne (4) za kutokomeza michezo haramu ya kubahatisha; kukusanya mapato yatokanayo na michezo ya kubahatisha ya jumla ya Sh bilioni 24.89;

“Kuendelea kuelimisha jamii juu ya athari hasi za michezo ya kubahatisha; na kusimamia uendeshaji wa Bahati Nasibu ya Taifa,” amesema Waziri Nchemba.

By Jamhuri