Mabingwa wa Dunia, timu ya taifa ya
Ufaransa, wameongoza kutoa wachezaji
wengi katika orodha ya wachezaji bora wa
(FIFA) wa kiume, huku katika nyanja ya
klabu, mabingwa wa Ulaya (Champions
League) Klabu ya Real Madrid wakiongoza
kutoa wachezaji wengi.
Mafanikio ya uwemo wa wachezaji katika
orodha hii kumechangiwa na mafanikio yao
waliyopata kutoka katika michuano ya
Champions League na Kombe la Dunia,
lakini pia mafanikio binafsi katika klabu zao.

1. Cristiano Ronaldo (Ureno/Real Madrid)
Amekuwa na mchango mkubwa kwa timu
ya taifa ya Ureno, kwa kuwa kinara kwa

kuivusha kuelekea Kombe la Dunia na
kufanikiwa kupiga mashuti 21 na
kufunga mabao 4 licha ya kuondolewa na
Uruguay katika hatua ya 16 bora.
Kwenye klabu alifunga mabao 15 katika
michuano iliyopita ‘Champions League’ na
kuibuka kinara wa ufungaji na kuisaidia
klabu kutwaa kwa mara ya tatu Champions
League, kwa kufunga magoli 44 msimu
uliopita katika mechi 44 na ‘assists’ 8.
2. Lionel Messi (Argentina/Barcelona)
Alifunga hat-trick katika mchezo wa kufuzu
Kombe la Dunia dhidi ya Ecuador, matokeo
yaliyoipeleka Argentina Urusi, licha ya
matokeo kuwa mabaya, alikuwa na kiwango
kibovu, akishuhudia wakiondolewa katika
michuano.
Kwenye klabu, alikuwa kinara wa ufungaji
kwenye ligi akiwa na magoli 36 na
kuiwezesha Barca kutwaa La Liga na katika
msimu uliopita Messi na Cr7 waligawana
ngome, Messi akitawala La Liga, huku Cr7
akitawala Champions League.
3. Kylian Mbappe (Ufaransa/PSG)
Huyu ni mchezaji bora chipukizi wa Kombe

la Dunia 2018 na kwa kuisaidia Ufaransa
kuwa mabingwa akivunja rekodi ya Pele ya
kuwa mchezaji mdogo kufunga mabao
mawili Kombe la Dunia tangu Pele afanye
hivyo mwaka 1958, lakini goli lake
pia kwenye fainali hizo likamfanya kuwa
mchezaji mdogo zaidi kuwahi kufunga
katika fainali za Kombe la Dunia, kwa
kufunga magoli 4.
Katika Klabu yake ya PSG alikuwa na
mchango mkubwa kwa kubeba ubingwa
wa Ligue 1, kwa kucheza michezo 27 na
kufunga magoli 13.
4. Luka Modric (Croatia/Real Madrid)
Mchango wake kwa timu ya taifa, hii ni
injini kwa timu ya Taifa ya Croatia, achilia
mbali kama kiongozi uwanjani amefunga
mabao 2.
Ngazi ya Klabu yake ya Real Madrid,
mipango ya mashambulizi yote
huanzia kwake, kwa mfano katika La Liga
peke yake Modric amepiga pasi timilifu kwa
wastani wa asilimia 90 msimu uliopita, huku
Champions League akiwa na asilimia 89.
5. Harry Kane (Uingereza/Tottenham)

Japo waliishia katika hatua ya nusu fainali
Kombe la Dunia, lakini Kane alikuwa kinara
wa magoli nchini Urusi akifunga magoli 6.
Alikuwa wa pili kwa ufungaji EPL, akiwa na
mabao 30 ndani ya dakika 3,083 alizocheza
EPL msimu uliopita huku akipiga
mashuti 76 yaliyolenga lango na kuifanya
Tot kumaliza nafasi ya 3 na kupata nafasi
ya kucheza Champions League msimu
ujao.
6. Mo Salah (Egypt/Liverpool)
Goli lake pekee dhidi ya Congo liliwapa
ushindi Misri kwenda Kombe la Dunia Urusi,
hii ni tangu mwaka 1990, lakini akashindwa
kung’ara katika michuano hiyo ya Dunia
nchini Urusi.
Alikuwa kinara wa mabao EPL akimaliza na
mabao 32 na kuisaidia Liverpool kumaliza
katika nafasi ya nne ya msimamo wa EPL
huku pia akiipeleka Liverpool fainali ya
Champions League kwa mara ya kwanza
tangu 2004/2005 huku akihitimisha
michuano kwa kufunga mabao 10 na
‘assists’ 4.
7. Kelvin De Bruyne (Ubelgiji/Man City)

Japokuwa waliishia katika hatua ya nusu
fainali Kombe la Dunia kwa kuondolewa
na Ufaransa, hata hivyo alionyesha ubora
wake akifunga goli 1 na akitoa ‘assists’ 2 na
kuisaidia nchi yake kumaliza nafasi ya tatu.
Katika mechi 38 alizocheza Manchester City
alifunga mabao 8 na kutoa ‘assists’ 16 na
kubeba Kombe la EPL huku akiwa katika
Champions League akitoa ‘assists’ 4 na
kwa ujumla ana ‘assists’ 21 na mabao 13.
8. Eden Hazard (Ubelgiji/Chelsea)
Katika Kombe la Dunia alikuwa miongoni
mwa wachezaji waliokuwa na kiwango cha
hali ya juu, akicheza dakika 518 na kuishia
hatua ya nusu fainali na kufunga
mabao 3 na ‘assists’ 2.
Japo Klabu ya Chelsea haikufanikiwa
kumaliza katika nafasi za juu EPL, lakini
walifanikiwa kubeba Kombe la FA na uwezo
wa Eden Hazard msimu uliopita umemfanya
kuwa lulu sokoni kwa
kufunga mabao 12 katika mechi 36.
9. Antoine Griezman (Ufaransa/Atletico
Madrid)
Alikuwa moja ya nguzo kwa timu ya taifa

ya Ufaransa kiasi cha kubeba Kombe la
Dunia nchini Urusi, katika
michezo 7 ambayo alicheza alifanikiwa
kufunga mabao 4 na kutoa ‘assists’ 2.
Ndani ya klabu walifanikiwa kubeba Kombe
la Europa huku akifunga mabao 2 katika
fainali vs Marseille, mabao 19 La Liga na
‘assists’ 9 huku wakimaliza nafasi ya pili
katika ligi.
10. Raphael Varane (Ufaransa/Real
Madrid)
Wasiokuwa na takwimu wanaweza
kushangazwa na uwepo wa Varane katika
orodha hii, hata hivyo alionyesha uwezo
mkubwa wa ulinzi kwa Ufaransa katika
Kombe la Dunia na bao moja alilofunga
dhidi ya Uruguay lilimpa kitu cha ziada.
Alikuwa na mchango mkubwa ndani ya
Klabu ya Real Madrid katika eneo la ulinzi
kiasi cha kubeba Kombe la Champions
League kwa mara ya tatu mfululizo.

By Jamhuri