Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Sensa akizungumza wakati alipofungua kikao cha kamati hiyo kwenye ukumbi wa hoteli ya Verde, Zanzibar Oktoba 11, 2022. Kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti Mwenza, Hemed Suleiman Abdulah.
Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Sensa wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ambaye pia ni  Mwenyekiti wa   kamati hiyo wakati alipofungua kikao cha kamati hiyo kwenye ukumbi wa hoteli  ya Verde, Zanzibar Oktoba 11, 2022. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti Mwenza, Hemed Suleiman Abdulah. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)